NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 16, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman aliyemaliza muda wa uwakilishi nchini Tanzania Mhe. Ali Bin Abdallah Bin Salim Al Mahrooq, Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Ali Al Mahrooq aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Ali Al Mahrooq (katikati) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi Nchini akiwa na Balozi Mdogo wa Oman hapa Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi (kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Ali Al Mahrooq (katikati) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Ali Al Mahrooq baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuaga akiwa amemaliza muda wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa katika picha na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe. Ali Al Mahrooq (kushoto) aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar,kuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi Nchini akiwa na Balozi Mdogo wa Oman hapa Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi (kulia).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Mhe.Ali Al Mahrooq aliyefika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. (Picha zote na Ikulu).
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Al Mahrooq alitumia fursa hiyo
kumuaga rasmi Rais. Dk. Mwinyi huku akisisitiza kuendelezwa ushirikiano
uliopo hususani katika sekta za kibiashara baina ya Oman na Zanzibar.
Aidha Balozi Al Mahrooq ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa kushirikiana na Oman wakati wa muda wake hapa nchini kwenye
maendeleo mbalimbali ikiwemo uimarishwaji wa sekta ya Elimu Zanzibar,
kukarabati majengo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar na miradi mingi ya
maendeleo.
Kwa Upande wake Rais. Dk Mwinyi amemshukuru Balozi Al Mahrooq na
kuishukuru Oman kwa ushirikiano mkubwa na kumtaka afikishe salam kwa
Sultan wa Oman, Mhe. Haitham Bin Tariq Al Said kumueleza Zanzibar iko
tayari na itaendelea kushirikiana na Oman katika sekta mbalimbali za
kibiashara na kijamii kwani Oman na Zanzibar zina historia kubwa na ya
kipekee.