Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mhasibu Mkuu wa Serikali, Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua Bi. Mtumwa Khatib Ameir kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Bi. Mtumwa Khatib Ameir ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Zanzibar.
Uteuzi huo ulianza tarehe 4 Agosti, 2021.