Rais Samia ana kwa ana na viongozi wa Chama cha TAWJA, TLS

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 11 Agosti, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji Joaquine De-Mello amempongeza Mhe. Rais Samia kwa kushika nafasi ya uongozi na kuwa Rais wa kwanza Mwanamke nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji Joaquine De-Mello, wakati alipoongoza Ujumbe wa Chama hicho, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 11 Agosti, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Jaji Joaquine De-Mello, wakati Ujumbe huo ulipofika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 11 Agosti, 2021. PICHA NA IKULU.

Mhe. Jaji De-Mello amesema Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA), kinafarijika na uongozi wake kutokana na mambo mbalimbali anayofanya ikiwa ni pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia kwa kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Amesema TAWJA iko tayari kushirikiana na Serikali katika kusimamia haki pamoja na kuhakikisha Serikali inafikia lengo la usawa wa kijinsia wa 50 kwa 50 katika ngazi mbalimbali za uongozi.

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amekishukuru Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA) kwa kazi nzuri inayofanya na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kutekeleza majukumu yao na amepokea changamoto zao na kuahidi kuzifanyia kazi.

Wakati huohuo, Mhe. Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambapo Rais wa Chama hicho Profesa Edward Hoseah amesema wameomba kukutana na Mhe. Rais ili kujitambulisha na kuelezea majukumu yao.

Profesa Hoseah amesema pamoja na mambo mengine, TLS ina jukumu la kumshauri Rais, Serikali, Bunge na Mahakama katika masuala mbalimbali ya sheria na utawala bora.

Aidha, Profesa Hoseah amemhakikishia Mhe. Rais Samia kuwa TLS iko tayari kuendelea kushirikiana na kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali ya kisheria.

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia ameishukuru na kuipongeza TLS kwa kazi nzuri inayofanya katika kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali.

Mhe. Rais ameihakikishia TLS ushirikiano wa kufanya nao kazi kwa karibu ili kuweza kutimiza majukumu yake pia amepokea changamoto zao mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Profesa Edward Hoseah wakati Ujumbe wa Chama hicho ulipofika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 11 Agosti, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Profesa Edward Hoseah, wakati Ujumbe huo ulipofika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 11 Agosti, 2021. (PICHA ZOTE NA IKULU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news