RC DKT. SENGATI KUWA MKALI UFUATILIAJI WA RASIMALI FEDHA ZA MIRADI

Na Anthony Ishengoma,Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Philemon Sengati amsema hatakuwa legelege katika kusimamia rasilimali fedha zinazotolewa na serikali au wananchi kwa ajili kutekeleza miradi ya maendeleo na hatasita kuchukua hatua kali kwa watendeji wabadhirifu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akisaidia kusogeza kifusi cha udongo kusaidia wanazengo wa Kijiji cha Mwamala wanaojitolea nguvu zao kuchimba shimo kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwamala Kishapu Mkoani Shinyanga.

Dkt. Sengati alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bw. Joseph Mkude kusimamia miradi kwa karibu kwasababu katika Wilaya yake kuna shida ya wizi na uzembe na baadhi ya watendaji hawana dhamira ya kufanya kazi kwa lengo la kutoa matokeo makubwa.

Dkt. Sengati alisema hayo jana kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa iliyofika Shule ya Sekondari Ukenyenge Wilayani kishapu kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na ukarabati wa miundombinu chakavu ya shule hiyo.

Dkt. Sengati alitoa agizo hilo kufuatia ziara ya ukaguzi wa miradi chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bw. Mabala Mlolwa kukataa taarifa ya Mkuu wa Shule aliyoitoa mbele ya kamati hiyo kuwa ukarabati wa chumba cha mahabara utagharimu kiasi cha shilingi milioni 30.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa akifungua maji ndani ya chumba ya cha mahabara ambacho kinafanyiwa ukarabati pamoja na kamati yake walipofika Shule ya Sekondari Ukenyenge kujionea maendeleo ya ukarabati wa mahabara hiyo jana Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa aliutaka uongozi wa shule na watendaji wa Wilaya ya Kishapu kuhakikisha kiasi hicho fedha kinatumika vizuri na kukarabati vyumba vitatu badala ya chumba kimoja ili kazi itakoyofanyika iendana na thamani ya fedha.

Aidha Bw. Mlolwa alioji matumizi ya fedha na kuonya kuwa wananchi watakata tamaa ikiwa hatutamia kiasi hicho cha fedha kukamilisha vyumba vitatu na kuwataka wafanye kazi hiyo kama ambavyo michango ya kujitolea ya wananchi inavyofanya vizuri katika ujenzi wa baadhi ya vyumba vya madarasa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude alihaidi kwenda sambamba na watendaji hao kwa kuwa katika maeneo mengine fedha kama kama izo zimekuwa zikitumiaka vizuri hata kuongeza ofisi ya walimu katika kiasi hicho cha fedha kinachotolewa na serikali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa akisaidia kusogeza kifusi cha udongo kusaidia wanazengo wa Kijiji cha Mwamala wanaojitolea nguvu zao kuchimba shimo kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwamala Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mkude aliomba kupatiwa orodha ya bidha na bei zilizoainishwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo hayo ili aweze kuzipatia kwa lengo la kujilidhisha na kuona baini tatizo liko wapi ili aweze kurekebisha mapungufu yaliyopo.

Aidha kiongozi huyo wa Wilaya alibainisha kuwa kama viongozi wangeachia suala hilo kupita bila kuoji kiasi kikubwa cha fedha kingebaki na kupata matumizi ambayo sio sawa nakuhaidi kulivalia njuga suala hilo.

Wakati huhuo Muhandisi wa Mkoa wa Shinyanga Francis Magoti aliongeza kuwa vifaa vionavyohitajika katika ukarabati wa mahabara hiyo ni vya kawaida na kumtaka muhandisi wa Wilaya Matoke Kyando kufanya kazi kwa karibu na shule hiyo kuhakikisha ufamisi unakuwa mzuri na unaoendana na thamani ya fedha.

Pamoja na kasoro hiyo kubainika pia ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga pia haikufurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mwaweja na kuomba Mkuu wa Mkoa kupeleka timu ya wataalamu kufanya uchunguzi zaidi kujilidhisha na matumizi ya rasilimali katika mradi huo.

Ziara ya Kamati ya Siasa imehitimisha kazi yake ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga ambayo imfanyika katika Halmashauri za Msalala, Kishapu, Ushetu, Kahama Manispaa, Halmashauri ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news