TAGCO, MAELEZO waanza kufuatilia utendaji kazi wa Maafisa Habari

 Na Mwandishi Wetu, Ulanga

Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano na Habari wa Serikali (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari -MAELEZO wametembelea Halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro kwa lengo la kufuatilia utendaji kazi wa Maafisa Habari na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha mawasiliano baina ya Serikali na wananchi.
Viongozi wa TAGCO na Idara ya Habari-MAELEZO wakiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, Andreas Whero katika ziara ya kikazi inayolenga kufuatilia utendaji kazi wa Maafisa Habari katika halmashauri za mkoa huo.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa TAGCO, Bw. Gerard Chami amesema kuwa dhamira na lengo kuu la ziara hii ni kufuatilia utendaji kazi wa Maafisa Habari na kufanya tathmini katika ngazi ya Halmashauri ili kuweza kutekeleza jukumu la kuisemea Serikali na wananchi waweze kujua ni kiasi gani Serikali inatekeleza yale iliyoyaahidi kila mmoja katika eneo lake la utendaji.

‘’Lengo hasa la ziara hii ni kufuatilia utendaji kazi wao, kubaini mafanikio yao kiutendaji na changamoto wanazokabiliana nazo ili kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja wakati wa tathimini ya utekelezaji wa majukumu yao ya kuhabarisha umma juu ya maendeleo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali,’’ amefafanua Bw. Chami.

Aidha, Chami ametoa rai kwa Maafisa Habari kuwa mbele katika kutangaza miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo kwani wananchi wanapenda kusikia kile kinachotekelezwa na Serikali yao.
Kwa upande wa mwakilishi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Bi. Beatrice Lyimo ametoa rai kwa Halmashauri ya Ulanga kuendelea kuimarisha redio ya Halamshari ya Ulanga ili iweze kuhabarisha wananchi wa Ulanga juu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na halmashauri hiyo kwani pia redio ni sehemu na moja ya chombo na kitendea kazi cha Kitengo cha Mawasiliano na Habari cha Halmashauri.

‘’Uwepo wa redio hii utasaidia kutangaza shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo zinazoendelea katika Halmashauri hii maana wananchi wanahitaji zaidi kujua miradi ya maendeleo inayoendelea ndani ya Halmashauri husika,’’ amefafanua Bi. Beatrice.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ulanga Bw. Andrea Whero pamoja na kazi nzuri anayoifanya Afisa Habari wa Halmashauri katika eneo la redio ya Halmashauri, ameahidi kuzichukua changamoto zilizobainishwa kumkabili Afisa Habari wa Halmashauri hiyo na kuzifanyia mpango wa utatuzi kwa lengo la kumuwezesha kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Aidha, Bw. Whero amepongeza jitihada zinazofanywa na Afisa Habari huyo za kuhabarisha umma licha ya changamoto zilizopo.

Ziara ya Viongozi wa TAGCO na Idara ya Habari - MAELEZO ni utekelezaji wa Maazimio ya Kikao Kazi cha Mwaka 2021 mkoani Mbeya katika kutembelea vitengo vya habari nchini ili kufuatilia utendaji kazi wa Maafisa Habari hao na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha mawasiliano kwani dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wanapata taarifa rasmi zilizo sahihi nakwa wakati za miradi ya maendeleo.


MUHIMU


UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news