Tazama tozo yako inavyoanza kufikisha vituo vya afya tarafa mbalimbali nchini





UJENZI WA VITUO VYA AFYA 150 NA UKAMILISHAJI WA VYUMBA VYA MADARASA 560 KUTOKA KATIKA TOZO YA MAWASILIANO

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imepokea fedha kutoka katika tozo ya Mawasiliano kiasi cha Shilingi Bilioni 22.5 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 90 katika Tarafa ambazo hazina vituo vya Afya na tarehe 23 Agosti, 2021 itapokea kiasi cha Shilingi biilion 15 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya 60 na hivyo kufanya jumla ya Vituo vya Afya vitakavyojengwa kutokana na tozo ya mawasiliano kuwa 150.

Halikadhalika OR-TAMISEMI tarehe 23 Agosti, 2021 itapokea tena kiasi cha Shilingi bilioni 7 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarsa 560 katika shule za Msingi na Sekondari nchini.

Kufuatia upatikanaji wa fedha hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuwa:-

1. Ujenzi wa Vituo vya Afya na ukamilishaji wa vyumba vya madarsa uanze mara moja ndani ya wiki mbili mpaka mwezi mmoja baada ya kupokea fedha za ujenzi na utekelezaji wa ujenzi usizidi miezi mitatu; 

2. Majengo yanayopaswa kuanza kujengwa kwa upande wa Afya ni Jengo la Wagonjwa wa Nje, Maabara na Kichomea Taka; 

3. Ujenzi wa miradi hii utumie Force account na sio Mkandarasi “Fedha hizi ni vyema zikarudi kwenye Jamii husika; na 

4. Vituo vya Afya vijengwe kwenye Makao Makuu ya Tarafa ambayo haina Kituo cha Afya na kama Tarafa hiyo ina Hospitali ya Halmashauri basi Halmashauri ichague Kata ya kimkakati ndani ya Tarafa hiyo kujenga Kituo cha Afya.

Imetolewa na;
   
Nteghenjwa Hosseah 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais – TAMISEMI
 20.08.2021

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news