NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Nyota wa Kikosi cha Yanga SC wameondoka leo kwenda nchini Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na msimu hadi itakaporejea kwa ajili ya tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 29, mwaka huu.
Wameondoka baada ya kutambulisha wachezaji wapya tisa wakiwemo makipa Eric Johola (Aigle Noir), Djigui Diarra (Stade Malien), beki wa kushoto, David Bryson (KMC ) na beki wa kulia Djuma Shabani (AS Vita).
Wengine ni winga wa kulia, Jesus Moloko (AS Vita), winga wa kushoto, Dickson Ambundo (Dodoma Jiji FC), washambuliaji Yussuf Athumani (Biashara United), Fiston Mayele (AS Vita) na Heritier Makambo (Horoya).
Awali uongozi wa Yanga SC umesaini mkataba wa ushirikiano katika nyanja mbalimbali na KCCA ya Uganda.
Mkataba huo unawafanya kuwa washirika wa tatu baada ya Sevilla ya Hispania na Raja Casablanca ya Morocco.