Chama cha Waendesha Mashtaka wa
Afrika Mashariki kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na jumla ya wanachama wa
nchi tano zikiwapo Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na
Kenya. Hadi kufikia hivi sasa chama hicho kimefanikiwa kuongeza
wanachama kutoka nchi nyingine jirani zikiwemo Somalia, Ethiopia,
Eritrea, Djibouti, Sudan, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Zambia, Malawi
na Msumbiji.