Pengine huenda sasa, Watanzania wengi wameanza kuchoshwa na kile wanachodai ni mipasho ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe, Josephat Gwajima kwa kuendelea kutumia madhabau takatifu kulumbana na mamlaka za Serikali hususani kuhusiana na chanjo dhidi ya janga la UVIKO-19.
MWANDISHI DIRAMAKINI anakusogezea kwa karibu chambuzi zilizotolewa huku zikiwa na maonyo kwa Askofu Gwajima kutoka kwa mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Thadei Ole Mushi huku Mheshimiwa Zitto Kabwe na Mchungaji Peter Msigwa wakichambua kupitia video fupi chini.
Ndugu Thadei Ole Mushi anamtaka Askofu Gwajima kutambua kuwa, Waziri wa Afya, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima anatumikia kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hivyo asidhalilishwe.
"Dkt.Dorothy yeye anatekeleza majukumu ya Kiserikali kwa mujibu wa Sheria.Hata kama aliwahi kukosea huko nyuma akarudi kurekebisha makosa yake sioni tatizo. Waziri yeye alikula kiapo cha kumtii Rais na ndicho anachokitumikia kwa uaminifu.Sasa yeyote anayemlaumu huyo hakumbuki hiki kiapo kabisa,"anafafanua Ole Mushi.
Mchungaji Peter Msigwa anafunguka
"Kwa jicho la nyama unaweza kufikiri Askofu Gwajima anapambana na Dorothy Gwajima yeye binafsi. Lakini kwa jicho la kitafiti ni kuwa Askofu Gwajima anamtumia Dorothy Gwajima kuipiga mamlaka teuzi. Hapa haihitaji Rocket science kuling'amua,"anaongeza Ole Mushi.
Zitto Kabwe afunguka
"Kwa bahati mbaya sana Waziri Gwajima ni kama vile wenzake, kwa maana ya mhimili wa dola wamemwachia sekeseke hilo la chanjo peke yake. Hii issue ni ya kitaifa na imebeba usalama wa nchi lakini, the way inavyojadiliwa inataka kufanywa kuwa ni issue ya kifamilia. Na leo waziri kwa kuwa anatumikia kiapo chake kadhalilishwa kabila lake la Kinyiramba,"anafafanua Ole Mushi.