Na Tito Mselem, Ruvuma
Imeelezwa kuwa, madini yote ni Rasilimali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yamewekwa chini ya uangalizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya watanzania wote.
Waziri wa Madini Doto Biteko (kulia) akizungumza jambo katika mgodi wa Lukarasi uliopo wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Saimon Msanjila.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko alipotembelea mgodi wa Lutarasi unaochimba madini ya dhahabu uliopo katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma
Akizungumza katika mkutano na wachimbaji wadogo, Waziri Biteko amewataka wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika mgodi huo kuwa waaminifu katika kazi zao na pia amemtaka mmilki wa mgodi huo Johnson Nchimbi kuwatendea haki wafanyakazi wake kwa kuwalipa stahiki zao kwa wakati na kwa kuzingatia makubaliano yao.
Aidha, Waziri Biteko amempongeza Nchimbi kwa kuwekeza fedha nyingi katika mradi wa uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu katika mgodi huo.
Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua shughuli za wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akizungumza jambo katika mkutano wake na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
“Kuna watu wanachanganya kati ya Haki Ardhi na Haki Madini hizi ni Haki mbili tofauti na kuna watu wanaamini Haki Ardhi inanguvu zaidi kuliko Haki Madini, hapana Haki zote ni sawa na zinasimamiwa na Serikali unapewa wewe Mtanzania kwa muda mfupi,” amesema Waziri. Biteko.
Pia, Waziri Biteko amesema kuna eneo kubwa kule Dar-Poli Wilaya ya Nyasa ambalo leseni yake imeisha muda wake, ambapo ameilekeza Ofisi ya Madini ya Wilaya ya Nyasa walifute ili Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya wapeleke vikundi vya watu wanaotaka kuchimba waombe leseni wachimbe ili walete maendeleo katika Mkoa wa wa Ruvuma.
"Mama yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuelekeza sisi wasaidizi wake tuje tutatue kero zote zilizopo katika maeneo yenu na tutahakikisha migogoro yote tunaipunguza au tunaimaliza kabisa," amesema Waziri Biteko.
Waziri wa Madini Doto Biteko (mbele katika), Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge (kulia) na (kushoto) Mmiliki wa Mgodi wa Lutarasi Johnson Nchasi wakitokea kwenye ukaguzi wa shughuli za wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu walioshiri mkutano wa Waziri wa Madini Doto Biteko wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Waziri wa Madini Doto Biteko kiwa na baadhi ya viongozi wakipewa maelezo nammiliki wa mgodi wa Lutarasi uliopo wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Pia, Waziri Biteko amemuhakikishia muwekezaji wa mgodi wa Lutarasi Johnson Nchimbi kupata msaada wowote atakao hitaji kutoka Serikalini ikiwemo kumuunganisha na mabenki yaliopo nchini ili apate mkopo na kuendeleza mgodi wa Lutarasi ambao utawaletea wananchi wa Ruvuma maendeleo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema, Nchimbi ni mchimbaji mdogo rukiki ambaye anahitaji kukua na amemtaka achangie ukuaji wa maendeleo ya eneo la Lutarasi ili iendane na uzalishaji uliopo katika eneo hilo ikiwemo uongezaji wa ajira na maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua shughuli za wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Saimon Msanjila katika ukaguzi wa mgodi wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wa Lukarasi uliopo wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Pia, Brigedia Ibuge amempongeza Waziri Biteko kwa kufanya ziara katika mkoa wa Ruvuma ambapo amemuahidi kutelekeza maagizo yote aliyoyatoa mkoani humo.
Awali Waziri Biteko alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kupokea taarifa ya mwenendo mzima wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini katika mkoa wa Ruvuma.