Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias John Kwandikwa afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias John Kwandikwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga amefariki dunia leo Jumatatu Agosti 2,2021 wakati akiendelea kupata matibabu kijini Dar es Salaam.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa amethibitisha.

"Nimepokea taarifa za msiba huu mzito kutoka uongozi wa CCM wilaya ya Kahama, Mpendwa wetu alikuwa anaendelea na matibabu jijini Dar es salaam,"amesema.

Wakati wa uhai wake,Kwandikwa alihudumu katika siasa za Tanzania kupitia Bunge tangu mwaka 2015 hadi 2020 kupitia Jimbo la Ushetu.

Aidha, Uchaguzi Mkuu wa 2020 alichaguliwa tena kuwawakilisha wananchi wa Ushetu, ndipo akateuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi.

Alihudumu nafasi ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kati ya mwaka 2017 hadi 2020. Hadi alipoteuliwa kuhudumu nafasi ya Waziri wa Ulinzi mwaka 2020. 

Nafasi ambayo iliongozwa kwa miaka 10 na Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambaye kwa sasa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, kufuatia kifo cha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Elias John Kwandikwa kilichotokea tarehe 2 Agosti, 2021 jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mhe. Kwandikwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga kutokana na mchango wake mkubwa katika utumishi wa umma.

“Tumempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi wa umma hautasahaulika, Kwandikwa alikuwa kiongozi shupavu ambaye alikuwa akitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu,"amesema Mhe. Rais Samia.

Mhe. Rais Samia amemtaka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na msiba huo.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amina.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaffar Haniu ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.



About Elias Kwandikwa


CURRICULUM VITAE – (CV)


SURNAME:

KWANDIKWA


FIRST NAME:

ELIAS


OTHER NAME:

JOHN


SEX:

MALE


MARITAL STATUS

MARRIED


DATE OF BIRTH

1ST JULY 1966


TRIBE:

SUKUMA


NATIONALITY

TANZANIAN


LANGUAGE SPOKEN:

SWAHILI/ENGLISH/SUKUMA


EDUCATION:


CERTIFICATE OF PRIMARY SCHOOL EDUCATION

Kisuke Primary School – Kahama (1977-1983)


CERTIFICATE OF SECONDARY SCHOOL EDUCATION

Mwenge Secondary School – Singida (1984-1987)


ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY SCHOOL EDUCATION (ACSSE)

Shinyanga Secondary School Shinyanga (1988-1990)


ADVANCED DIPLOMA IN ACCOUNTANCY

Institute Of Finance Managements- IFM ,1999


MASTERS OF BUSINESS ADMINISTRATION (MBA)

Eastern and Southern African Management Institute –ESAMI ,2015


LEADERSHIP AND POLITICAL RESPONSIBILITIES

Minister-Defence and National Service- Dec 2020 -today

Deputy Minister – Works 2017 – 2020

Member of Parliament 2015-2020

CCM – District Central Committee Member – Kibaha Town 2012-2015

CCM - District Central Committee Member – Kahama District 2015-2020

CCM – Regional Executive Committee Member Shinyanga Regional 2015-2020

Public Investment Committee Member – Tanzania Parliament 2015 – 2017

ALAT Executive Committee Member 2015-2020


EMPLOYMENTS - PROMOTIONS


NATIONAL AUDIT OFFICE – TANZANIA (NAOT)

Assistant Examiner of Accounts II (1990-1995)

Assistant Examiner of Accounts I (1995-1997)

Examiner of Accounts III (1997-1999)

Auditor III (1999-2003)

Auditor II (2003-2004)

Senior Auditor (2004-2005)

Chief Accountant (2005-todate)

Second Auditor Incharge – Kibaha

Audit Branch (1999-2000)

Second Auditor Incharge – TRA-VAT (2000-2005)

Head, Finance and Account Unit (Chief Accountant)

NATIONAL Audit Office(2005 – 2015)


MEMBER OF PARLIAMENT

DEPUTY MINISTER

Parliament of Tanzania – 2015-2020

Ministry of Works, Transport and Communication 2017-2020


PROFESSIONAL QUALIFICATION

Advanced Diploma in Accountancy, IFM -1999

Certified Public Accountant (CPA-T), NBAA-2004

Associate Certified Public Accountant ,NBAA-2007


PROFESSIONAL ASSIGNMENTS

Trainer/Facilitator – Auditor Qualifying Examination – Morogoro Oct., 2004

Facilitator on a Training to Standing Parliamentary Accounts Committees on understanding of the CAGs Reports Financial Statements analysis and interrogation skills (April-May, 2008)


IN-SERVICE TRAINING/EXAMINATION

Lower Government Accountancy -

Certificate (Presidents Office, 1995)

Higher Government Accountancy -

Certificate (Presidents Office, 1995)

Auditors Qualifying Examination Certificate (Presidents Office , 2004)


COMPUTER KNOWLEDGE

Computer Basic Course Certificate

Institute of Finance Management Accounting Association - 1998

Microsoft Office 2000 Fundamentals SCI (TZ) Ltd -2004

Other sills – Ms Word; Ms Excel, Ms Works, Outlook express, PowerPoint etc.


TRAINING/SEMINARS/WORKSHOPS:


End users Training on epicor (IFMIS) Integrated Financial Management Information System

One and half month intensive training by Soft Tech Consultants – Dar es Salaam – Tanzania 2005


Problems and Prospect encountered in adoption of IFRSs and ISASs

One day intensive Seminar Conducted by NBAA – DSM Tanzania (Septmber, 2005)


Financial Prevention Training

One week seminar on financial prevention course conducted by IFEX Training London at Uganda 2006


Generating Economic Growth and stability world wide

One week intensive seminar organized by Stability worldwide World Congress of Accountants by IFAC Istanbul – Turkey2006


Meeting challenges of Public Management Reform in East Eastern and Southern African Seminar

One week intensive Seminar organized by Association of and Southern Africa Accountant General at Maseru Lesotho -2006


Accounting Standards for small and Medium – sized entity Seminar

One day Seminar Conducted by National Board of Auditors and Accountant (NBAA) -April, 2007


Wholesale adoption of IFRS and ISA Seminar

Two day Seminar organized by NBAA at Arusha, Tanzania- 2007


Improving Accountability regarding the use of Public Resources

One day Seminar organized by Tanzania Association of Accountants (TAA) Dar es Salaam Tanzania -April, 2007


Audit tests, Quality and Risk Managements

One week seminar organized by the National Audit Office – Tanzania at Dar es Salaam -May, 2007


Leadership Development Programme (Leaders of change with Global Perspective)

One week training on leadership skill organized by Tanzania Global Development Learning

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news