500 WAJITOKEZA MAONESHO YA MADINI GEITA

Na Mutta Robert,Geita

Wafanyabiashara,wachimbaji wakubwa na wadogo,wajasiriamali,makampuni,taasisi za umama na sekta binafsi zipatazo 500 zimejitokeza kushiriki katika Maonesho ya Teknolojia ya Uwekezaji katika Sekta Madini mjini Geita.
Hayo yameelezwa na mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu maonesho hayo yatakayoanza tarehe 16 Septemba,2021.

Amesema, wadau mbalimbali wa sekta ya madini nchini kutoka kwa wanaojihusisha na uchimbaji mdogo,wa kati na mkubwa, lakini pia sekta zisizo za madini,wapato 500 watakuwa na mabanda ya kuonesha shughuli zao na watu zaidi ya 20,000 watatembelea maonesho hayo.

Amefafanua kuwa, maonesho hayo mdhamini mkuu ni kampuni ya dhahabu ya Geita (GGML), lakini pia kuna wadau wengine wadogo wadogo ambao pia wameshiriki kuchangia udhamini.

Mgodi wa GGML licha ya kudhamini maonesho ya Mwaka huu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini katika Mkoa wa Geita pia inatoa zaidi ya sh.Bilioni 9.2 kila mwaka kutoka kwenye mpango wake wa huduma kwa jamii (CSR) kwa ajili ya Halmashauri mbili ya Geita Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa ajili ya elimu,afya,michezo,elimu na huduma nyingine za kijamii.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amefafanua kuwa, maonesho hayo yatafunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kufungwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philipo Mpango.

Ameongeza kuwa, mwaka jana mchango wa sekta ya Madini katika pato la taifa ilichangia kwa asilimia sita na mkoa wa Geita unazalisha madini ya dhahabu kwa asilimia 40 nchini na kwamba maonesho hayo watu watajifunza teknolojia mbalimbali katika sekta hiyo.

Ameeleza kuwa, licha ya mchango wa sekta ya madini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 6 maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 hadi 2025 inaelekeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa kufikia asilimia 10.

Aidha, amewata wananchi,wafanyabiashara,wachimbajiwakubwa na wadogo wa madini,wauzaji,wajasiriamali,makampuni na taaasisi za umma na za sekta binafsi kujitokeza kushikiriki maonesho hayo.

Senyemule amesema, kamati ya ulinzi na usalama imejipanga kuimarisha usalama katika kipindi chote cha maonesho hayo kwa siku kumi za maonyesho ambapo kwenye eneo hilo kinafunguliwa kituo cha polisi cha muda, lakini pia vikosi vingine vya usalama ili kuhakikisha mali za washiriki na wananchi ziko salama muda wote.

Maonesho hayo ya teknolojia ya uwekezaji katika sekta ya madini katika mkoa wa Geita ni ya nne tangu kuanzishwa kwake ambayo yalianzishwa kwa lengo la kubadilisha teknolojia na kupata taarifa sahihi katika mnyororo mzima wa sekta husika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news