Ajali ya basi yaua, yajeruhi 33 mkoani Kagera

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Watu wanne wamethibitika kupoteza maisha na wengine 33 kujeruhiwa.
Ni baada ya basi la Kampuni ya Fikosh lililokuwa likitoka Mkoa wa Mwanza kuelekea mkoa wa Kagera kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa Nyangoye uliopo katika Manispaa ya Bukoba Mkoa wa Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Moses Machali amesema kuwa, basi hilo lenye namba za usajili T710 BXB wakati linapata ajali lilikuwa likitokea Mkoa wa Mwanza na lilikuwa limebakiza umbali mfupi kuingia katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Bukoba.

Amesema kuwa, taarifa hizo ni za awali, na kwamba kama kutakuwa na ongezeko la vifo au majeruhi watatoa taarifa baadae.

"Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali na idadi ya abiria waliokuwemo, tunaomba subira taarifa rasmi itatolewa baadae ikikamilika," amesema.

Aidha,Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amethibitisha taarifa hiyo na kueleza kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha watatu ni watu wazima na mmoja ni mtoto mdogo.

Kamanda huyo amesema,maiti zimepelekwa na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera na majeruhi wamepelekwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu.

Pia amesema, uchunguzi unaendelea na taarifa za watu walioshuhudia wamedai gari hilo lilipoteza mwelekeo baada ya kumaliza kona katika mteremko huo na kuanguka pembezoni mwa barabaraba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news