Na Hadija Bagasha, Tanga
Anord Mtei ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kilindi asilia amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Kilindi akikabiliwa na tuhuma za kumfyeka mwenzake sehemu za siri.

Cpl Makono alieleza kuwa, mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 29,mwaka huu na kwamba alimkata Matonya Luberege sehemu zake za siri kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
Alidai kuwa kitendo hicho kilimsababishia mlalamikaji wa kesi hiyo maumivu makali mwilini mwake.
Adidai kuwa, kitendo alichokifanya mshitakiwa ni cha kikatili na ambacho pia ni kosa na kinyume na sheria.
Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka hilo na kurejeshwa rumande baada ya kukosa watu wa kumdhamini.
Kesi hiyo imepangwa kuja mahakamani hapo kwa mara ya pili kwa ajili ya kuanza kusikilizwa Septemba 24, mwaka huu.