NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mkuu wa mkoa wa Geita, Rosemary Staki Senyamule ametangaza rasmi usiku huu kuwa, kesho saa tatu asubuhi ataongoza wananchi wote wa Geita kwenda kuchangia damu katika banda la Waandishi wa Habari wa mji wa Geita (GMG) ,lengo likiwa ni kuokoa maisha ya wanawake wanaopungukiwa damu wakati wanajifungua na wanaopata ajali hasa bodaboda.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule (katikati),Makamu Mwenyekiti wa GMG,Mutta Robert (kulia) na Magdalena Gumbu Mtaalam kutoka kitengo cha damu salama Hospitali ya Mkoa wa Geita (kushoto).
"Mimi Rosemary Staki Senyamule, Mkuu wa Mkoa wa Geita. Keshosho tarehe 25/09/2021 nategemea kwenda kutoa damu ili kuokoa maisha ya wanawake wanaopungukiwa damu wakati wa kujifungua pamoja na watu wanaohitaji damu kwa kupata ajali wakiwemo bodaboda.
"Nakuomba uniunge mkono ili tuokoe maisha. Hatujui na sisi tutahitaji damu lini na nani atatuokoa. Mhali ni eneo la maonesho EPZ Bombambili na muda ni kuanzia saa 3.00 hadi saa 11.00 jioni. GEITA YA DHAHABU, UTAJIRI NA HESHIMA. Karibu tuupe Heshima Mkoa wetu,"ameeleza usiku huu.