DC Hanafi Msabaha awaonya wafugaji,wakulima vinara wa migogoro Uvinza

Na Anneth Kagenda

WAKULIMA na Wafugaji Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wamepigwa marufuku kuacha migogoro na mapigano badala yake wametakiwa kukaa meza moja na kutafuta suluhuu ya matatizo hayo na si mapigano na ugomvi usiokuwa na tija.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Hanafi Msabaha (aliyenyoosha mkono) akifafanua jambo.

Mkuu wa wilaya hiyo, Hanafi Msabaha amepiga marufuku migogoro kati ya wafugaji na wakulima mara baada ya kufanya mkutano kati ya pande hizo mbili na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo wakulima hao na wafugaji.

DC Hanafi amesema kuwa, ni wakati mwafaka kwa wakulima na wafugaji kutumia Serikali za vijiji na kata katika maeneo yao kumaliza migogoro baina yao kuelekea msimu wa kilimo unaokuja ili kuisaidia Serikali katika kukabiliana na kesi hizo.

DC Hanafi, amezitaka pande zote kufanya shughuli zao kwa ushirikiano kwani kila mmoja ana haki na kusema kuwa, mkulima ana haki yake na mfugaji ana haki yake hivyo hakuna anayetakiwa kunyanyaswa kwenye maeneo yao.

"Wafugaji ng'ombe wanalisha kwenye mashamba ya wafugaji na kwa namna moja hama nyingine wengine wanapigwa virungu na kuumizwa,"amesema DC Hanafi na kuongeza;

"Kwa stahili hii basi niwaombe tuheshimiane kila watu kwenye nafasi yao, maana yake ni kwamba akitokea mfugaji akalisha mazao ya mkulima hata kwa bahati mbaya, ni vyema wakakutana na kuzungumza ili masuala hayo yaweze kuisha kwa makubaliano,"amesema.

Hata hivyo, wananchi katika wilaya hiyo walimuomba Mkuu huyo wa wilaya kulivalia njuga suala la mivutano iliyopo kati ya pande hizo mbili yaani wafugaji na wakulima na kuweza kilipatia ufumbuzi kwa madai kuwa limedumu kwa mda mrefu bila kupata mwafaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news