Na Hadija Bagasha, Tanga
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa ametoa onyo kali kwa wazazi na walezi wenye tabia za kuwarubuni watoto wao wasifanye vizuri katika mitihani ya kuhitimu elimu yao ya msingi, kwani kufanya hivyo kunapelekea kushindwa kufikia ndoto zao za kupata elimu.


DC Mgandilwa amesema kuwa, Wilaya ya Tanga na mkoa kwa ujumla kuna changamoto kubwa kwenye masuala ya elimu kwa kuwa wapo wazazi wanaodiriki kuwarubuni watoto wao wafanye vibaya kwenye mitihani yao ili wasiweze kujiendeleza na elimu ya mbele.
Hivyo aliwataka wazazi kubeba wajibu wao wa kuhakikisha watoto wanaporudi nyumbani wanasimamia maendeleo yao na kuwafuatilia kwa ukaribu ili kuwafanya watoto wenyewe waamini kwamba shule ni muhimu katika maisha yao.
“Ndugu zetu wazazi wilaya yetu ya Tanga na Mkoa wetu Tanga tuna changamoto kubwa katika masuala ya elimu wazazi, wanafunzi kumekuwa na mtihani mkubwa sana wanafunzi wanaanza shule lakini kumaliza inakuwa mtihani wapo wazazi wanaodiliki kuwaambia watoto wafanye vibaya wanapokuwa wanafanya mitihani yao ili watoto wasiendelee na elimu yao ya mbele,”amesema Mgandilwa.

“Serikali haina uwezo wa kufanya kila kitu inahitaji msaada wa Private sekta kwajili ya kuondoa baadhi ya changamto ambazo zipo kwenye maeneo yetu kwahiyo kitendo cha kuwekeza katika sekta hii hapa Tanga mimi niwatie moyo na niwaahidi kuwa serikali ya Mkoa wa Tanga itawapa ushirikiano kila mtakapohitaji,”alisema DC Mgandilwa.
"Niwapongeze kwa uamuzi mzuri Kitendo cha kuamua kuufanya wa kuwekeza Taasisi hii hapa Tanga lakini pia kuwekeza kwenye elimu tunajua taasisi zetu hizi za shule ni huduma lakini pia mnaziendesha ili kupata chochote leo hii nimeshuhudia huduma nzuri mnayoitoa kwa watoto wetu niwatie moyo muendelee hivyo hivyo,”alisema DC Mgandilwa.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa shule hiyo imeweka walimu wa kutosha wenye weledi wa kufundishwa masomo yote kama unavyoelekeza mtaala wa elimu ya msingi Tanzania, lakini pia shule hiyo imefanikiwa kutekeleza malengo yake kwa asilimia 99 ikiwemo kusaidia pamoja na serikali katika kutoa elimu bora miongoni mwa malengo mengine.
“Tumefanikiwa kuwa na ufaulu mzuri na unaoridhisha katika mitihani ya ndani ya kujipima na ya nje kama mock na mitihani ya taifa Necta ya darasa la nne na la saba katika awamu zilizopita ambapo kwa awamu hii wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba 2021, ni 68, wamefanikiwa kumaliza elimu ya msingi,”amesema.