DC Siriel Mchembe atoa rai kwa World Vision

Na Hadija Bagasha,Tanga

Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Siriel Mchembe amesema vitendo vya watoto wa kike kuchezewa na mimba za utotoni vinakuwa tatizo kwenye wilaya yake kutokana na jamii kuvifumbia macho na kumalizana nyumbanii.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo kwenye kikao cha wadau wa Shirika la Maendeleo la World Vision cha tathimini ya maendeleo ya miradi iliyofanywa kwenye eneo hilo.

DC Mchembe amelitaka Shirika hilo la World Vision kuhakikisha linaweka mikakati ya kuendelea kusaidia kuwalinda watoto wa kike, lakini pia na wa kiume ambao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ulawiti ili kukomesha vitendo hivyo.

"Mimba za utotoni nimeona hapa mnatusaidia kutoa elimu hapa ni nyingi,lakini pia tumeona watoto wa kiume wanaingia kwenye changamoto za kuharibiwa, lakini tumeona hata watoto wa kike wa miaka 10 wakiingia kwenye mahusiano yale mimi siyaiti mahusiano ni ubakaji kwa mujibu wa sheria za kumlinda mtoto wa kike ipo haja ya kuendelea kukemea," "amesistiza Mchembe.

Mkuu huyo wa wilaya ameliomba shirika hilo kupitia mpango wa World Vision wajikite kuangalia jamii kwa kuwa ndani ya miaka minne waliokuwepo wilayani humo imewatosha kuifahamu jamii, lakini pia hata kufahamu utamaduni wa mahali waliopo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi ya matenki ya maji eneo la Magamba wilaya humo Mratibu wa mradi kutoka World Vision Tanzania Kanda ya Mashariki,Allice Mbaga amesema kuwa wametekeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jamii ikiwemo miradi ya visima.
Allice Mmbaga ambaye ni Mratibu wa Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya mashariki akizungumza mara baada ya kutembelea matenki yaliyofadhiliwa na shirika hilo.

Mratibu huyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuhakikisha wanatunza miradi waliyofikishiwa kwa kuwa imetumia gharama kuwa na hivyo ili wanufaike ni lazima waitunze.

Mmbaga amesema kuwa, Tarafa ya Magamba ni eneo ambalo limekumbwa na changamoto kubwa ya maji na ndio maana walipokaa na jamii wakasema wao kama shirika washikirikiane na jamii ili kuwajengea matenki matatu.

Alisema mategemeo yao wananchi na wanafunzi wataweza kunufaika na maji safi hayo ambapo matenki hayo kila moja lina ukubwa wa ujazo wa lita elfu 30 yaliyogharimu jumla ya milioni 87.5.

Shirika hilo kwenye miradi ya afya, maji, usafi, na lishe limesaidia jamii kwa asilimia 45, wakati kwa upande wa elimu likitumia asilimia 24 huku kwenye ufadhili wa mambo mtambuka likisaidia jamii kwa asilimia 29.

Walimu pamoja na wananfunzi wamelishukuru shirika hilo la World Vision kwa kuwawezesha kuwasaidia na kutatua changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa kikwazo katika masomo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news