Kilindi yapewa miezi mitatu zahanati ikamilike

Na Hadija Bagasha, Kilindi

MKUU wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Abel Busalama ameipa miezi mitatu halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha zahanati ya Kijiji cha Kimembe inatoa huduma kwa wananchi.

Sanjari na agizo hilo, Mkuu huyo wa wilaya amelishauri Shirika la World Vision Tanzania, kubadili taratibu zake za ujenzi wa miradi ili kabla hawajaikabidhi kwa serikali, iwe imekamilika kwa asilimia 100.
Habari picha ni Mkuu wa wilaya Kilindi Abel Busalama akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na watendaji wa shirika la world vision Tanzania. (Picha na Hadija Bagasha).
Akizungumza wakati akikagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na shirika hilo katika Tarafa ya Mgera, mkuu huyo wa wilaya alisikitishwa na taarifa kwamba World Vision wamekamilisha zahanati ya kijiji cha Kimembe miaka minne iliyopita, lakini hadi sasa haijaanza kutoa huduma kwa wananchi.

Amesema, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaposhirikiana na wafadhili mbalimbali katika miradi ya maendeleo lengo lake ni kuiwezesha jamii inapata huduma kwa karibu na kuboresha ustawi wao.

"Tatizo lililopo ni utayari wa halmashauri katika kupokea miradi ya World Vision. Halmashauri ibadilike na ipokee miradi hii na kuweka bajeti, jengo linachakaa kabla ya kutumika, ni hasara," amesema Mkuu huyo wa wilaya kwa masikitiko.

Kufuatia hatua hiyo Busalama ameiagiza halmashauri kuhakikisha zahanati hiyo katika kipindi cha miezi mitatu ijayo inafanya kazi kwa kulifanyia ukarabati na kukamilisha mahitaji muhimu ikiwemo usajili.

"Kutokana na mazingira haya nagoma kulikagua jengo hili hadi hapo mtakapolikamilisha na kuanza kazi,"amesema Busalama.

Zahanati hiyo ujenzi wake ulianzishwa na wanakijiji kwa lengo la kutatua changamoto inayowasumbua ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya matibabu kwa kusafiri kufikia vituo vya afya vya vijiji jirani.

Kwa mujibu wa wanakijiji wa Kimembe, wanalipa sh. 7,000 kwa usafiri wa pikipiki kusafirisha wagonjwa wanaohitaji huduma za matibabu katika Kituo kipya cha Afya huko Kwediboma, na Mswaki.

Mkuu wa Wilaya ambaye alitembelea zahanati hiyo akiongoza wajumbe wa Kamati ya Uratibu ya Mradi wa World Vision Mgera wa Eneo la Mgera (PCC), ikijumuisha wadau, kutembelea miradi iliyotekelezwa na shirika katika miaka miwili iliyopita.

Mradi huo ulianzishwa na wanakijiji na World Vision na hadi kukanilika kwake imetumia sh. milioni 74.

Mkuu wa wilaya alisema kuwa, haikubaliki kwamba jengo ambalo lililenga kupunguza changamoto za kiafya za jamii limekaa bila kazi kwa miaka minne wakati wanajamii katika eneo hilo wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufikia huduma za afya.

“Halmashauri inahitaji kubadilisha mtazamo wake kwa miradi iliyojengwa na washirika. Ninaambiwa wataalam wa halmashauri wanahusika katika utekelezaji wa miradi hiyo. Inamaanisha kwamba kimantiki Halmashauri inatambua mradi huo na inapaswa kuwa tayari kuudumisha au kuuendesha baada ya kukabidhiwa,”Busalama alisema.

Mkuu huyo wa Wilaya ambaye pia alitembelea Kituo cha Ufundi Stadi kilichojengwa na World Vision ambacho sasa kina wanafunzi wawili tu. alisema ripoti zinaonyesha kuwa Halmashauri ilihusika kutoka hatua za mwanzo katika ujenzi wa kituo, hivyo ni mantiki kwamba walipaswa kujiandaa kuchukua miradi hiyo.

"Inasikitisha kuona uwekezaji huu wote uko hapa bila matumizi yoyote yenye tija," alisema akiwashawishi wahusika kukamilisha usajili wa kituo hicho na kutoa wito kwa wazazi kupeleka watoto katika kituo hicho kinachofundisha ufundi cherahani.

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya Dkt.Nasra Lichika, alisema awali zahanati hiyo haikuwa imekamilika vyoo ambavyo kwa sasa vipo isipokuwa haina sehemu ya kutupia kondo la nyuma la wazazi (Plaster Kitt) na kichomea taka (baning Chember).

Mratibu wa Mgera AP, Modest Kessy alisema kuwa, shirika limetumia sh.bilioni 2.09 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Kilindi kwa zaidi ya miaka miwili.

Alisema kuwa, fungu kubwa la fedha hizo zimetumika katika miradi ya maji, usafi wa mazingira, afya na lishe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news