Naibu Waziri Gekul atoa maagizo kwa maafisa michezo

 NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,   Mheshimiwa Pauline Gekul ametoa wito kwa maafisa michezo wa mikoa na halmashauri kusimamia kwa karibu shughuli za michezo shuleni na kwenye taasisi zilizopo katika maeneo yaoMhe. Gekul ametoa wito huo leo Septemba 13, 2021 wakati wa kikao kazi na maafisa michezo na maafisa utamaduni wa mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

"Ni jukumu lenu kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata muda wa kutosha kushiriki katika shughuli za michezo ikiwa ni pamoja na kukimbia mchakamchaka kila siku asubuhi ili kuimarisha afya zao na kuwafanya wakakamavu,"amesema Mheshimiwa Gekul.

Katika ziara yake ya siku moja mkoani humo, Mheshimiwa Gekul pia alishiriki mazoezi ya jogging pamoja na ufunguzi wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wakike wa shule za sekondari na vyuo katika Jimbo la Nsimbo (Lupembe Cup) sambamba na kutoa zawadi kwa washindi wa ligi hiyo kwa mwaka 2021.
"Ninampongeza sana Mheshimiwa Lupembe kwa kuanzisha mashindano haya na hasa kwa uamuzi wake wa kuwa na mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa kike, niwaombe waheshimiwa wabunge na wadau wa michezo kuiga mfano huu ili kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa watoto wetu wa kike,"amesema Mheshimiwa Gekul.

Ligi ya Jimbo la Nsimbo (Lupembe Cup) imedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Anna Lupembe ambapo imeshirikisha timu kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi ya kata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news