NA MWANDISHI MAALUM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 29 Septemba, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Mhe. Tony Blair, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu Chamwino jijini Dodoma. (Picha na Ikulu).
Mhe. Tony Blair ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya
Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change)
amemshukuru na kumhakikishia Mhe. Rais Samia kuwa taasisi yake inaunga
mkono jitahada mbalimbali anazochukua katika kuwaletea maendeleo
wananchi wa Tanzania.
Amesema ili kuwa na mafanikio ya haraka
katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni muhimu kuwa na taarifa
sahihi ambazo zitawezesha ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Mhe. Tony Blair kwa kukutana nae na kumjulisha ufuatiliaji na uratibu wa masuala yanayofanywa na taasisi yake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania.
Aidha, Mhe. Rais Samia amesema kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa vipaumbele vyake kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
Tags
Habari