Rais Samia ateua viongozi mbalimbali leo Septemba 25,2021

NA GODFREY NNKO

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, alichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka.

Kabla ya uteuzi huo, Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Afrika Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Vilevile, Rais Samia amemteua Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO.

Rais Samia amemteua Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kabla ya uteuzi, alikuwa Meneja wa Kanda Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TANESCO.

Aidha, Michael Minja ameteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati. Kabla ya kuteuliwa, Minja alikuwa Mkurugenzi Mkuu TIPPER.

Vilevile, Rais amemteua Felschemi Mramba kuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amewahamisha Watumishi Waandamizi watano kutoka TANESCO kwenda Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo watapangiwa majukumu mengine.

Waliohamishwa ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji, Khalid James; Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Masoko, Mhandisi Raymond Seya na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji, Mhandisi Isaac Chanje.

Wengine ni Nyelu Mwamaja (Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi) na Amos Ndegi (Mwanasheria wa TANESCO).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news