Salim Alaudin Hasham awapa faraja wanakijiji Muhuwesi

Na Hadija Bagasha

WANANCHI wa Kijiji cha Muhuwesi kilichopo Kata ya Muhuwesi wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma wamemshukuru mwekezaji Salim Alaudin Hasham kwa kuwajengea zahanati katika kijiji chao kwani wamekuwa na changamoto hiyo kwa miaka mingi.
Wakizungumza mara baada ya zahanati hiyo kuwekewa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021, Luteni Josephine Mwambashi wamesema akinamama wamekuwa wakipoteza maisha nyakati za kujifungua kutokana na changamoto ya mazingira ya zahanati ya awali, hivyo kwa sasa wana uhakika wa afya zao kwani watapata huduma bora.

Mwekezaji wa eneo hilo, Salim Alaudin alisema ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 80 na ameamua kufanya hivyo baada ya kuona adha wanayoipata wananchi wa eneo hilo pindi wanapohitaji huduma hiyo.

Naye Luteni Josephine Mwambashi alimpongeza mwekezaji huyo na kusema yeye amekuwa mfano wa kuigwa kwa wawekezaji wengine ambao wanawekeza katika maeneo ya wananchi wawe na kipaumbele cha kuwasaidia kwa kuwatatulia changamoto zinazowakabili.

Zahanati hiyo inatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya 20,000 wanatoka kwenye vitongoji 20 ambao hapo awali walikuwa wanapata shida kupata huduma za afya kutokana na eneo la zahanati ya awali kuwa chakavu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news