Tundu Lissu, wenzake wafutiwa kesi ya uchochezi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefuta kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, Tundu Lissu na wenzake watatu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Lissu na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002 ya Tanzania.

Wengine waliokuwamo katika kesi hiyo walikuwa ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news