Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akimuonesha baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo katika jarida la Utalii kutoka Tanzania Waziri wa Utalii wa Hispania, Maria Illerakabla baada ya kumkabidhi zawadi ya majarida yanayoelezea utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini mara baada kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano wa 64 Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku nne katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde.(Picha zote na WMU).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi ya Kitabu cha misitu kinachoelezea fursa za uwekezaji katika maeneo ya misitu nchini Mhe. Ngobitizitha Ndlovu (kushoto) mara baada kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku nne katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( katikati ) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Utalii na Mambo Kale Zanzibar, Mhe.Lela Mussa Mohamed (kushoto) pamoja na Waziri wa Utalii wa Morroco, Mhe.Nadia Fettah ( kulia) mara baada kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku nne katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiagana na Waziri wa Utalii Cape Verde, Mhe. Carlos Santos ambapo wamekubaliana katika kubadilishana uzoefu katika kukuza utalii.