Ukikashifu viongozi umekwenda na maji

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI imeviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake kuwakamata na kuwachukulia hatua kali wanaotumia mitandao ya kijamii kuwakashifu viongozi wa Serikali na kusema kuwa ni kinyume cha sheria.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene amesema hayo leo jijini Dodoma kwenye mkutano wake na waandishi wa habari huku akisema hali hiyo haitavumilika na kwamba kuanzia sasa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa wale wote watakaoendelea na tabia hiyo.

Simbachawene amesema, kila mwananchi anapaswa kusimamia matumizi sahihi ya mitandao ukiwemo wizi unaofanyika pamoja na uhuru wa kutoa mawazo ambao wengi wamekuwa wakiutumia vibaya kwenye mitandao ya kijamii.

"Namuagiza Kamishina wa polisi nchini Camillus Wambura kushughulikia wale wote wenye malalamiko ya kutoa fedha ili kesi zao zishughulikiwe na jeshi la polisi kwenye kesi za makosa ya jinai,"amesema .

Aidha,Waziri Simbachawene amebainisha kwamba zaidi ya shilingi milioni 500 hadi Bilioni 1 fedha za wananchi wanyonge, wastaafu huibiwa na matapeli kwa njia ya mitandao.

"Kuna wananchi hulipishwa fedha pindi wanapoenda kulalamika kupotelewa na vitu vyao ikiwemo simu za mkononi na baadhi ya polisi kuwadai wananchi fedha ,nawaomba polisi kuacha mara moja tabia hiyo na mkasimamie haki na maadili,"amesisitiza Simbachawene.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news