Usalama ni jambo muhimu katika maeneo ya kazi-Waziri Biteko

Na Tito Mselem-WM

Imeelezwa kuwa, usalama na afya katika sehemu za kazi ni jambo muhimu linalopaswa kupewa kipaumbele kuliko jambo lolote lile hususan katika maeneo ya migodi.
Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati) akizungumza jambo kwenye Kikao Kazi cha kujadili masuala ya usalama, afya na baruti kilichofanyika Septemba 13, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi na kulia Kaimu Mwenyekiti wa Tume ya Madini Janet Ruben.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi akizungumza jambo kwenye Kikao Kazi cha kujadili masuala ya usalama, afya na baruti kilichofanyika Septemba 13, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma, kushoto ni Kamishna wa Madini Dkt. Abdul Rahman Mwanga.
Hayo ameyabainisha Waziri wa Madini Doto Biteko katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha kujadili masuala ya usalama, afya na baruti kilichofanyika Septemba 13, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma.

Waziri Biteko amesema lengo la kikao kazi hicho ni kujadili namna bora ya kulinda usalama, afya na baruti ili mwisho wa siku Wizara na Taasisi zake ziweze kufikia lengo la kukusanya bilioni 650 iliyopangiwa na Serikali na kuwaacha watu wakiwa salama.

Waziri Biteko amesema zinapofanyika shughuli za uchimbaji madini lazima athari za mazingira zitokee, hivyo amewataka wakaguzi wa migodi kote nchini kuziona athari kabla hazijatokea ambapo amesema ajali yoyote inapotokea lazima viashiria viwe vimeshabainishwa na wakaguzi wa migodi kabla ya ajali kutokea.

“Bora tukose hela lakini watu wetu wawe salama, nendeni mkakague kwa uangalifu na uaminifu, na pia msikague kwenye taka sumu pekee kagueni kote ikiwemo migodi ya kati na migodi ya wachimbaji wadogo, tusiwe bize na masuala ya dharura, hakikisheni mnafatilia ili mjue aina ya uchimbaji salama,” amesisitiza Waziri Biteko.
aziri wa Madini Doto Biteko (kushoto) akizungumza jambo kwenye Kikao Kazi cha kujadili masuala ya usalama, afya na baruti kilichofanyika Septemba 13, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma, (kulia) Kaimu Mwenyekiti wa Tume ya Madini Janet Ruben.

Aidha, Waziri Biteko amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Dkt. Abdul Rahman Mwanga kuwa Kamishna wa Madini na kueleza kuwa, jambo zuri kuteuliwa mtu ambaye ametoka miongoni mwao.

“Rais wetu anataka kila Wizara na Taasisi za Serikali zijisimamie zenyewe, zifanye maamuzi yaliyo sahihi, ukiona Rais kateua kiongozi kutoka miongoni mwenu ujue mnaaminika asingeshindwa kuteua mtu kutoka mahali pengine, endeleeni kufanyakazi kwa uaminifu ili kufanikisha kukusanya maduhuli tuliyopangiwa na kukuza uchumi wa nchi yetu,” amesema Waziri Biteko.
Kamishna wa Madini Dkt. Abdul Rahman Mwanga akizungumza jambo katika kikao hicho.
Naye, Kaimu Mwenyekiti wa Tume ya Madini Janet Ruben, amempongeza Waziri Biteko kwa kukubali kuhudhuria kikao hicho na amemuahidi kwamba, atahakikisha maelekezo yote aliyoyatoa yanafanyiwa kazi ili mwisho wa siku lengo makusanyo ya bilioni 650 yafanikiwe na yaendane na usalama wa afya za watu.
Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Wizara, Tume ya Madini pamoja na Maafisa Madini wa Mikoa yote Tanzania baada ya Kikao Kazi cha kujadili masuala ya usalama, afya na baruti, kilichofanyika Septemba 13, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma

“Kikao hiki kitasaidia wakaguzi wote wa migodi nchini ili waweze kutambua viashiria vya vihatarishi katika maeneo ya kazi na kuona namna bora ya kuvipunguza kama sio kuvimaliza kabisa ili tulinde usalama na afya za watu wetu,” amesema Ruben.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news