NA MWANDISHI MAALUM
Mwandishi wa habari wa Global TV, ambaye kituo chake cha kazi ni jijini Dodoma, Mohamed Zengwa na wenzake wawili wamepata ajali mbaya ya gari leo Jumanne, Septemba 21, 2021 katika Kijiji cha Usimba, wilaya ya Uyui mkoani Tabora.






Watu wote watatu waliokuwa kwenye gari hiyo, hawajaumia sana zaidi ya kupata majeraha madogo madogo na hali zao zinaendelea vizuri ambapo wamekwenda hospitali kwa ajili ya vipimo matibabu zaidi.
Zengwa na wenzake hao, walikuwa wakisafiri kuelekea mkoani Kigoma kikazi.



Uongozi wa Diramakini Blog unajumuika na wafanyakazi wote wa Global Publishers Ltd pamoja na Dar Mpya kuwapa pole ndugu zetu hao kwa ajali hiyo.
Pia tunamshukuru Mungu kwa kuwanusuru kutokana na ajali hiyo mbaya na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye majeraha waliyoyapata ili warejee kuungana na familia zao na shughuli zao za ujenzi wa Taifa. (GP).