Walia ngo’mbe kuvimba, kupasuka miguu hadi kufa

Na Derick Milton, Meatu

Wafugaji wa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, wale wanaopakana na pori la akiba la Maswa na Hifadhi ya Taifa Serengeti wameeleza tatizo kubwa ambalo linatesa mifugo yao hasa ngo’mbe wao kushambuliwa na magonjwa mengi ya ajabu.
Mmoja wa wafugaji wa Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu akizungumza wakati wa mkuatno wa wafugaji wa wilaya hiyo na Mkuu wa mkoa huo, David Kafulila (hayupo pichani). (Picha na MWANDISHI DIRAMAKINI)

Wamesema kuwa magonjwa hayo yamesababisha ngo’mbe wao kufa wengi, huku wakibainisha kuwa ugonjwa ambao unawatesa zaidi ni mifugo yao kuvimba mwili mzima, kupasuka kwato, kuvimba mapafu pamoja na kutoa udenda.

Wafugaji hao wamezungumza hayo mbele ya Mkuu wa mkoa huo, David Kafulila wakati wa kikao chake na wafugaji hao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashuari ya wilaya hiyo.

Walisema kuwa, magonjwa hayo yamesababisha ngo’mbe wao wengi kupungua kutokana na kufa, huku wakidai ugonjwa wa kuvimba mwili pamoja na kupasuka kwako ndiyo umekuwa tatizo kubwa zaidi.

Walieleza kuwa, licha ya kuwepo kwa tatizo la malipo, lakini changamoto ya magonjwa hayo ndiyo kubwa zaidi hivyo wameioba Serikali kuwasaidia upatikanaji wa chanjo ya haraka ili kinusuru mifugo yao.

“Nilikuwa na ngo’mbe 80, lakini mpaka sasa nimebaki na ngo’mbe 37 tu, wengine wote wamekufa kutokana na magonjwa hayo, tunaomba sisi wafugaji hasa tunaopakana na hifadhi Serikali itusaidie,”amesema Shoka Felesi mfugaji.

Naye Hunge Hunge amesema kuwa, mbali na magonjwa, changamoto nyingine ni ukosefu wa majosho pamoja na malambo ya kunyweshea mifugo yao, ambapo wameiomba Serikali kuwatatulia kero hizo.

"Tunayo shida kubwa ya ukosefu wa majosho, ndiyo maana mifugo yetu inapata magonjwa mara kwa mara, hatuna majosho, lakini hata chanjo hatupati kwa muda mrefu,”amesema Hunge.

Kwa upande wake Afisa Mifugo wa halmashauri hiyo, Hussen Nyenye amekiri kuwepo kwa magonjwa hayo, ambayo alieleza yanasababishwa na mwingiliano uiliopo kati ya mifugo na wanyama kutoka hifadhini.

“Tatizo ni wafugaji wetu wengi kupeleka mifugo yao kwenye hifadhi, ndiyo maana wanapata magonjwa mbalimbali, lakini tumekuwa tukitoa chanjo ila wanaojitokeza wachache na kwa mwaka huu bado hatujatoa chanjo,”amesema Nyenye.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa, David Kafulila alimtaka mkurugenzi wa halmashuari kumpatia taarifa ya hadhari inayotokana na magonjwa hayo ili kujua ukubwa wa tatizo ili aweze kuomba msaada kutoka wizarani.

“Waziri wa Mifugo anatoka mkoa wa Simiyu, leo nitamweleza tatizo hili ili kuona wanaweza kutusaidia vipi kwa haraka kutatua shida hii, lakini nipate taarifa ya ukubwa wa tatizo hili,”amesema Kafulila.

Katika kikao hicho wakulima waliiomba Serikali kuanzisha mkakati wa upandaji wa nyasi za kisasa ili kuweza kukabiliana na changamoto ya malisho ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu ya ufagaji wa kisasa.

Wafugaji hao wamesema kuwa, wao wako tayari kupata mbegu hizo kwani wameona suluhisho la malisho si kuongezewa maeneo ya malisho bali ni kufuga kisasa ikiwemo kupanda nyasi.

Kutokana na ombi hilo, Mkuu wa mkoa amesema Serikali ipo tayari, ambapo aliagiza halmashauri kuhakikisha mbegu bora za nyasi zinapatikana na wakulima waanze kupewa ili wapate malisho ya mifugo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news