Waziri Mchengerwa aelekeza kuwashusha vyeo maafisa utumishi hawa

Na James K. Mwanamyoto, OR-Utumishi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaelekeza watendaji wa ofisi yake kufanya ufuatiliaji ili kuwashusha vyeo Maafisa Utumishi katika Taasisi za Umma walioshindwa kutekeleza agizo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hasssan la kuwapandisha vyeo watumishi wenye sifa za kupanda madaraja.
Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo leo wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Mhe. Mchengerwa amesema, Afisa Utumishi yeyote aliyezembea na kusababisha Watumishi wa Umma kutopandishwa madaraja achukuliwe hatua kwa kushushwa cheo na kuhamishwa kituo cha kazi ili iwe ni fundisho kwa wengine wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo.

“Fanyeni upembuzi na kuwaondoa Maafisa Utumishi wote waliobainika kutotekeleza wajibu wa kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa stahiki, kwani nimekuwa nikipokea malalamiko toka kwa watumishi wa taasisi mbalimbali,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa, ofisi yake ilifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha taarifa za kiutumishi zilizotumwa na waajiri zinafanyiwa kazi kwa lengo la kuwapandisha vyeo watumishi husika, hivyo amewapongeza watendaji wa ofisi yake kwa kutekeleza vema wajibu wao.

Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa, Mhe. Rais anawajali sana Watumishi wa Umma na ndio maana alitoa agizo la kuwapandisha vyeo katika kipindi ambacho mijadala ya bajeti Bungeni ilikuwa ikiendelea jambo ambalo katika hali ya kawaida isingekuwa rahisi kutekelezeka.

“Mhe. Rais anatambua kuwa nguzo ya Serikali kiutendaji ni Watumishi wa Umma hivyo haiwezi kufanya vizuri iwapo haitowajali watumishi wake na ndio maana aliagiza wapandishwe madaraja,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda akitoa neno la utangulizi kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa, mara baada ya waziri huyo kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali mara baada ya kufungua kikao kazi cha watendaji wakuu hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa ofisi yake, mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika amemshukuru Mhe. Waziri kwa kukubali wito wa kukutana na Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali na kumuahidi kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa.

Dkt. Shindika amemhakikishia Mhe. Mchengerwa kuwa Watendaji Wakuu hao wa Wakala za Serikali watahakikisha wanahimiza uwajibikaji kwa Maafisa Utumishi wao ili waendane na kasi ya kiutendaji ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amehimiza uwajibikaji kwa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali ili waweze kuendana na Kaulimbiu ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya KAZI IENDELEE.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news