NA MWANDISHI MAALUM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amepongea hatua iliyochukuliwa na Kampuni ya ORYX Enegies na Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) ya kusaini Mkataba wa Hiari wa Hali Bora ili kuendelea kuboresha mazingira ya wafanyakazi ili kuleta tija katika nafasi zao.
Hafla hiyo ilifanyika Septemba 24, 2021 na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa TUICO, Bw. Boniphace Nkakatisi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gesi ya ORYX,Benoit Aramari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya ORYX, Kalpesh Mehta na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri (ATE), Dkt. Aggrey Mulimuka pamoja na wafanyakazi wa kampuni hizo jijini Dar es Salaam.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja0ToFfOOpEToPHbLTHm6gC3vvIbN4_BMCiWrTxHrXCGixfiSakLROhVuxFlABxk06O4STpqUCQB0D7Vr6bWa4EyVid_mzVZqBgdrwOrTjooTJxk-HBNaLZj668lB1b7ymbyhBSSkZYiE/s16000/tuico+na+oryx.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEja0ToFfOOpEToPHbLTHm6gC3vvIbN4_BMCiWrTxHrXCGixfiSakLROhVuxFlABxk06O4STpqUCQB0D7Vr6bWa4EyVid_mzVZqBgdrwOrTjooTJxk-HBNaLZj668lB1b7ymbyhBSSkZYiE/s16000/tuico+na+oryx.jpg)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka wakishuhudia zoezi la uwekaji wa saini za mkataba wa hiari wa hali bora baina ya Menejimenti ya Makampuni ya ORYX Energies na Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO). Wa kwanza kushoto ni Bw. Kalpesh Mahta anayefuta ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ORYX, Bw. Benoit Aramari ni katika hafla fupi iliyofanyika Septemba 24, 2021 ofisi za ORYX jijini Dar es Salaam.
Waziri ameeleza kufurahishwa na makubaliano hayo kwa kubainisha faida zitakazopatikana kwa wafanyakazi ikiwemo kuongeza hali bora za wafanyakazi na kuongeza tija kwao.
“Ninafarijika sana kushuhudia waajiri wa Makampuni ya ORYX mnavyowajali wafanyakazi na kuchukua hatua kama hii ya utiaji saini wa mkataba wa hali bora bila ya kusukumwa na mtu yeyote hakika ninawapongeza sana,”amesema Waziri.
Waziri alisema kuwa, Makubaliano ya Mkataba wa Hali bora waliofikia ni hatua nzuri ya utekelezaji wa Sheria za kazi hususani Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 na Kanuni zake za mwaka 2007 (the Employment and Labour Relations Act No.6 of 2004 and the Code of Good Practice) Rule, 2007 (GN No. 42 ya tarehe 16TH Feb, 2007). Sheria hii na Kanuni zake zinaweka muongozo wa utaratibu na njia za kufuatwa na masuala muhimu ya kuzingatiwa katika kufanya majadiliano mahala pa kazi.
Aidha, aliwaasa wafanyakazi kuendelea kutumia fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa juhudi na ubunifu mkubwa ili kuwa na matokeo chanya katika kampuni hiyo.
“Wafanyakazi mtapata ziada ya vitu vingi msibweteke badala yake muwe na bidii na ushirikiano wa karibu ili tuendelee mbele badala ya kurudi nyuma,”alisisitiza
Naye Katibu Mkuu wa TUICO Bw. Boniphace Nkakatisi alieleza furaha yake kwa hatua hiyo na kuwaasa waajiri wengine kuona umuhimu wa kuwa na mikataba hii ili kuboresha utendaji kazi kwa wafanyakazi
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/P3.JPGAAAAAAAA.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/P4.JPGAAAAAAAA.jpg)
“Tunapoingia mikataba kama hii inasaidia kuboresha vipengele mbalimbali vya kisheria na vinavyotokana na mazingira ya kazi na kuleta afya na ustawi kwa masuala haya,”alisema Nkakatisi
Aliongezea kuwa, makubaliano haya yanaleta hali ya kuaminiana, kupunguza manung’uniko kazini, kupunguza migogoro na kuendeleza umoja na mshikamano baina ya menejimenti na wafanyakazi.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni za ORXY Bw. Benoit Aramari alishukuru Serikali kujali mazingira ya wawekezaji nchini na kuitumia nafasi hiyo kuendelea kuipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu yenye dhamana na masuala ya Kazi na Ajira nchini kwa kuona umuhimu wa kushuhudia makubaliano hayo na kuahidi kuendelea kushirikiana na kufanya kazi katika misingi na sheria za kazi zilizopo.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/P5.JPGAAAAAAAAAAAAA.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/P6.JPGAAAAAAAAAA-1.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/P7.JPGAAAAAAAAAA-2.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/P8.JPGAAAAAAA.jpg)
Akitoa neno la shukurani Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt.Aggrey Mulimuka alipongeza Waziri kuona umuhimu na kushuhudia zoezi hilo kwa kuzingatia wingi wa majukumu aliyonayo.Alipongeza Menejimenti na Wafanyakazi kwa kutambua uwepo wa Chama cha Wafanyakazi na kuweka makubaliano haya yanayoashiria uhai wa kampuni na kusema hatua hiyo inafaa kuigwa na wengine.