Yanga SC yawapiga Simba SC pale pale TP Mazembe walipofanya yao

NA GODFREY NNKO

Dakika 90 za Mchezo dhidi ya Simba SC na Yanga SC zimemalizika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

Ni katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo Yanga SC wameichapa Simba SC bao 1- 0.

Dakika 13 ya mchezo,Yanga SC kupitia kwa mshambuliaji wake Fiston Mayele alipiga shuti kali lililomaliza hesabu.

Kichapo cha leo kinakumbushia alichofanya Baleke Jean dakika ya 84 katika dimba hilo kwa kuwapa TP Mazembe ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Simba SC.

Ni katika tamasha la Simba Day Septemba 19,2021 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Tamasha hilo ambalo lilijaza maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo kutoka maeneo ya Msimbazi, licha ya kufungwa mashabiki walionekana kuridhika na kiwango cha wachezaji wao.
Aidha, kuridhika kwao, huenda Yanga SC wameitumia nafasi hiyo kujiimarisha.

Shuti la Mayele lilimshinda mlinda mlango wa Simba Aishi Manula.

Kwa matokeo haya Yanga wanachukua taji la Ngao ya Jamii.

Yanga SC ambao walikuwa Wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika, bado wana maumivu makali baada ya mbio zao kuhitimishwa nchini Nigeria.

Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi wa zaidi ya bao 1-0 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Pia ugenini nchini Nigeria, Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 2-0.

Ni katika mechi ya marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Adokiye Amiesimaka mjini Port Harcourt, Nigeria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news