Azam FC yajiandaa kutoa dozi kwa Pyramid FC

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Wanalambalamba, Azam FC wameendelea kujiweka sawa kuelekea mchezo mgumu dhidi ya Pyramid FC ya Misri.

Mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam ikiwa ni mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Hii ikiwa ni raundi ya pili katika mkondo wa kwanza.

Matajiri hao watarusha karata yao, Oktoba 16,2021 ambapo kwa mjibu wa taarifa za Azam Fc na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF ) zimeeleza kuwa mchezo huo utachezwa huku mashabiki 2,000 wakiruhusiwa kutokana na janga la virusi vya Covid-19.

Akizungumzia mchezo huo, Afisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa, matarajio makubwa kwa timu hiyo ni kufanya vizuri kwenye kila mchezo ambao watacheza kutokana na uwepo wa wachezaji wazuri pamoja na benchi la ufundi makini.
Mbali na uwanja wa kisasa, Azam FC inatajwa kuwa miongoni mwa klabu chache duniani ambazo zinamiliki mabasi ya kifahari likiwemo basi hili jipya aina ya Mercedes Benz Irizar i6S Plus, basi kama hili pia linatumiwa na baadhi ya timu kubwa duniani ikiwemo Liverpool FC na Real Madrid. (Picha na AzamFC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news