BARRICK YAANZISHA MAABARA YA KWANZA YA PHOTONASSAY BARANI AFRIKA KATIKA MGODI WA BULYANHULU

NA MWANDISHI MAALUM

Kampuni ya Dhahabu ya Barrick, kwa kushirikiana na kampuni ya MSALAB Ltd, zimefanikiwa kuanzisha katika mgodi wa Bulyanhulu nchini Tanzania maabara ya kisasa inayotumia mtambo wa Chrysos PhotonAssay kupima kiwango cha madini kwa eksirei.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow akimwonyesha Naibu Waziri wa Madini,Profesa Shukuru Manya ramani ya mgodi wa Bulyanhulu wakati wa hafla ya kuzindua maabara ya kisasa ya kupima madini katika mgodi wa Bulyanhulu.

Maabara hii ni ya kwanza na ya aina yake barani Afrika na katika uendeshaji wa shughuli za Barrick duniani.

Mbinu hii mpya inatoa uchambuzi wa haraka,salama na sahihi zaidi wa madini ya dhahabu, fedha na elementi nyinginezo za ziada kwa kutumia kipimo kisichoharibu mazingira cha sampuli kubwa na wakilishi zaidi ndani ya dakika mbili tu, jambo linalowezesha mabadiliko ya haraka katika suala la taarifa muhimu za uendeshaji wa shughuli za kampuni ambazo zinachochea ufanisi wa hali ya juu kabisa katika mnyororo mzima wa thamani katika uchimbaji madini.
Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukuru Manya (wa tatu kulia), Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow (wa pili kulia) wakikata utepe kuzindua maabara ya kisasa ya kupima madini katika mgodi wa Bulyanhulu. Kulia ni mjumbe wa bodi ya Twiga Mineral,Casmir Kyaki. Wengine ni viongozi wa serikali mkoani Shinyanga
Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow (kulia) akiongea na Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukuru Manya wakati wa hafla ya uzinduzi wa maabara ya kisasa ya Bulyanhulu.
Wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi wa maabara ya kisasa ya kimataifa wakibadilishana mawazo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick ,Mark Bristow na Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukuru Manya.

Mfumo huu unaleta mbadala endelevu zaidi wa njia za jadi za kutumia moto ambao si rafiki kwa mazingira,usiotumia kemikali na hivyo,unapunguza wa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa ya ukaa na taka hatarishi.

Akiutambulisha mfumo huo mpya kwa vyombo ya habari kwenye mgodi wa huo, Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow amesema kuwa, hiyo ilikuwa sehemu ya jitihada endelevu za kampuni za kutaka kutumia uvumbuzi wa kiteknolojia katika kuhakikisha kwamba shughuli zake zinaendeshwa kwa umahiri,kunakuwa na usalama na usalama kazini na mazingira yanatunzwa vizuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news