Hawa ndiyo wanafunzi 10 Bora Mtihani wa Darasa la Saba 2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Eluleki Evaristo Haule ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani ya Darasa la Saba 2021.
Hayo ni kwa mujibu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ambapo amehitimu shule ya msingi St.Anne Marie iliyopo mkoani Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo sita waliyotahiniwa.

Ameyasema hayo leo Oktoba 30,2021 wakati akitangaza matokeo hayo.

Pia alimtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Happy Joseph Deus kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mkoa wa Mara na nafasi ya tatu ikienda kwa John Chacha Charles kutoka Twibhoki.

Aliyeshika nafasi ya nne ni Joshua Mahende Jacob kutoka shule ya msingi Twibhoki iliyopo Mara pia, Eva Sebastian Chengula kutoka shule ya msingi Fountain of Joy ya Dar es Salaam ameshika nafasi ya tano, Joctan Samwel Matara kutoka Twibhoki ameshika nafasi ya sita.Matokeo yote soma hapa>>>

Barnaba Jumanne Magoto kutoka shule ya msingi Twibhoki ipo Mara ameshika nafasi ya saba, Rahma Ombi Juma kutoka shule ya Mtuki Highland iliyopo Dar es Salaam ameshika nafasi ya nane na nafasi ya tisa ni Juliana John Shimbala kutoka St Joseph’s nafasi ya kumi ameishika Jackline Manfredy kutoka shule ya Masaka iliyopo Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news