Na Happiness Shayo-WMU
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti itaendelea kuchangia miradi ya maendeleo katika vijiji saba vinavyoizunguka hifadhi hiyo ili kuinua uchumi wa wananchi wanaoshi katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo kwenye ziara ya Mawaziri 8 wa Kisekta leo.
Amesema kuwa kutokana na wananchi wa vijiji hivyo kutunza vizuri hifadhi hiyo, Serikali itaendelea kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Mwaka huu wa fedha tumetenga fedha za ujenzi wa madarasa mawili katika kijiji cha Kisangula, nyumba mbili za waganga na bwawa la kunyweshea mifugo katika kijiji cha Nyansulula na ukarabati wa bwawa katika eneo la Machocho.
Pia, Mhe. Masanja ameongeza kuwa Serikali itajenga kituo cha afya , nyumba za waganga na madarasa mawili katika kijiji cha Mbalibali, nyumba za waganga mbili, katika kijiji cha Tamkeni na madarasa mawili katika kijiji cha Nyambuli.