JKCI waongezewa ujuzi wa kutumia mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi


Mkufunzi wa kutumia mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) kutoka nchini Afrika Kusini Linda Veale akiwafundisha wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) (hawapo pichani) namna ambavyo mashine hiyo inavyoweza kufanya uchunguzi na vipimo mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mafunzo ya namna ya kutumia mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) wakati wa mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijifunza kwa vitendo namna ya kuunganisha vifaa vya kumuunganisha mgonjwa na mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa kutumia mashine ya kuusaidia moyo kufanya kazi kwa kiwango cha juu (Intra-aortic balloon pump) kutoka nchini Afrika Kusini Linda Veale akiwaonesha wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ambavyo mashine hiyo inavyofanya kazi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. (Picha na JKCI).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news