Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Daniel Baran Sillo akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati akisalimiana na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Zainabu Chaula na ujumbe wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TCRA Oktoba 12, 2021.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Daniel Baran Sillo akipokea maelezo ya ukaribisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Killimbe mara baada ya Ujumbe wa Kamati hiyo kuzuru TCRA kukagua masuala mbalimbali ya mawasiliano ikiwemo usimamizi wa Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS-Telecommunications Traffic Monitoring System). Kamati hiyo ilipokelewa Oktoba 12, 2021 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, watendaji wa Wizara na Menejimenti ya TCRA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Daniel Baran Sillo akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mara baada ya kuwasili na ujumbe wa kamati anayoiongoza kwenye ofisi hizo kwa lengo la kukagua masuala mbalimbali ya Mawasiliano ikiwemo usimamizi wa Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS-Telecommunications Traffic Monitoring System). Anaeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari(mkabala) na Mkurugenzi wa Bodi ya TCRA Dkt. Jones Kilimbe.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati walipotembelea Ofisi za TCRA kukagua masuala mbalimbali ya Mawasiliano ikiwemo usimamizi wa Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS-Telecommunications Traffic Monitoring System).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti baada ya kupokea hoja na maswali kutoka kwa wajumbe hao waliopozuru TCRA mnamo Oktoba 12, 2021 kukagua masuala mbalimbali ya Mawasiliano ikiwemo usimamizi wa Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS-Telecommunications Traffic Monitoring System); Wajumbe hao wamepongeza utendaji kazi wa TCRA na kutoa mapendekezo ya maboresho zaidi kwa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa na Menejimenti ya Mamlaka.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika mjadala wa pamoja na ujumbe wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Menejimenti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakijadiliana masuala mbalimbali ya mawasiliano na Menejimenti ya TCRA mara baada ya kutembelea mifumo ya mawasiliano ukiwemo mfumo wa Usimamizi wa Mawsiliano ya Simu. (Picha zote na TCRA).