Makamu wa Rais Tanzania awashukuru wazee nchini

NA MWANDISHI MAALUM

Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni mlezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango leo Oktoba 4, 2021 amezungumza na wazee wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, mazungumzo yaliofanyika katika viwanja vya Karimjee.
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasili katika viwanja vya Karimjee kuzungumza na wazee wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam leoe Oktoba 4, 2021.

Dkt. Mpango ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wazee wote nchini kupitia wazee wa Dar es Salaam kwa kuendelea kutoa ushauri, malezi na kulinda mila na desturi za nchi. 

Amesema mchango wa wazee nchini ni mkubwa kwani wao ndio waliopigania kuondoka kwa matabaka yaliokuwepo kipindi cha ukoloni na kusaidia katika kuleta uhuru wa pamoja na kuijenga nchi baada ya uhuru.

Amesema, taifa litaendelea kuenzi mchango waliotoa wazee kwa wakati wote walipolitumikia na kuahidi kuendelea kutumia ushauri wa wazee katika uongozi wake hapa nchini.

Aidha, Mlezi huyo wa Mkoa wa Dar es salaam ameagiza viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha wanafanya ziara na kusikiliza kero za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi wa haraka na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.
Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmshauri kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wazee wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es salaam katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.Oktoba 4, 2021.

Amewasihi wanachama wa CCM katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2022 kuwapa nafasi viongozi wenye sifa na wanaojali maslahi ya taifa ili kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Amesema ni muhimu Chama Cha Mapinduzi kuendelea kulinda rasilimali zilizopo ndani ya chama pamoja na kuhakikisha wanajenga vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia ili CCM iweze kujiendesha wakati wote.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameagiza Madawati ya wazee katika vituo vya kutolea huduma za Afya kufanya kazi kwa mujibu wa maelekeo na miongozo iliotolewa ili kuondoa changamoto zinazowakabili wazee wanapofika kupata huduma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, Hemed Mkali amesema wazee wanatambua juhudi zinazofanywa na serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Aidha, amempongeza mlezi wa chama Mkoa wa Dar es salaam kwa kutambua umuhimu wa wazee na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika juhudi za kuleta maendeleo ya Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news