NA MWANDISHI MAALUM
SPIKA wa Bunge Job Ndugai, amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri kupendana na kufanya kazi kwa kushirikiana kwani hivi sasa wapo baadhi yao ambao wanachukiana.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Mawaziri na Manaibu waziri wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.
Ndugai amewataka kuwa na ushirikiano katika kazi maana itawasaida wao katika kutekeleza majukumu yao hivyo msipopendana hamuwezi kuleta maendeleo katika sekta mnazosimami.
“Tunafahamu kuna baadhi yenu Waziri na Naibu wake hawapatani lazima tufanye kazi kwa ushirikiano kwani mwisho wa siku serikali yetu ni moja na huwezi jua kesho itakuwaje,”amesema Ndugai.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa,akizungumza wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa Mawaziri na Manaibu waziri wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Uongozi kwa Mawaziri na Manaibu Waziri wakimsikiliza Spika wa Bunge Job Ndugai,(hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Mawaziri na Manaibu waziri wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Aidha, amewakumbusha Mawaziri hao kuwa Dodoma ndiyo makao makuu ya serikali hivyo shughuli zote zinapaswa kufanyika hapa na siyo vinginevyo.
“Ukienda Marekani kama shughuli ni ya kufanyika Carfonia haita fanyika katika mji mwingine lakini ukienda Kenya shughuli ya kufanyika Nairobi haita fanyika Kisumu hivyo lazima tutekeleleze hili tusiwafanye hadi mabalozi waone kuwa kuhamia Dodoma siyo ‘issue,"amefafanua Ndugai.
Waziri wa Viwanda na Biashara,Prof.Kitila Mkumbo,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Washiriki kwa Spika wa Bunge Job Ndugai,(hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Mawaziri na Manaibu waziri wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyoandaliwa na taasisi ya Uongozi yaliyofanyika jijini Dodoma.
Kwa upande wake,Waziri wa Viwanda na Biashara,Prof.Kitila Mkumbo,ametoa neno la shukrani kwa niaba amesema kuwa watatekeleza kwa vitendo yale yote walijifunza katika mafunzo hayo.
Tags
Habari