Mawaziri waiongoza Kamati ya Bunge kukagua ujenzi wa jengo la makao makuu ya Uhamiaji jijini Dodoma


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, wakati alipokuwa anawasili na Wajumbe wa Kamati yake kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Uhamiaji, jijini Dodoma, leo Oktoba 27, 2021, linalojengwa na SUMA JKT. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika katika eneo la mradi wa ujenzi wa makao amkuu ya Uhamiaji jijini Dodoma, leo. Wapili Kushoto meza kuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu, na wapili kulia ni Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Stergomena Tax.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Jeshi la Uhamiaji katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Stergomena Tax, Waziri Simbachawene, na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (wapili kushoto), na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT), Meja Jenerali, Rajabu Mabele, wakati walipokuwa wanakagua mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Jeshi la Uhamiaji kabla ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kulikagua jengo hilo, jijini Dodoma, leo. Jengo hilo linajengwa na SUMA JKT.
Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt. Stergomena Tax (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, wakati alipokuwa anawasili katika mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Uhamiaji, jijini Dodoma, leo Oktoba 27, 2021, kabla ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, haijawasili katika eneo hilo kulikagua jengo hilo linalojengwa na SUMA JKT. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news