Mwinjilisti Alphonce Temba ashangazwa na unyenyekevu, usikivu wa Rais Samia, asema baada ya kuibua hoja Bandari Kavu Kwala mwanga mpya umeanza kuonekana

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba anemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kiongozi mwana mama imara na wa mfano ambaye ameingia katika historia ya nchi yetu kama mwanamke wa kwanza pekee aliyepata kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sambamba na kutumika kwa kuonyesha njia ya kiongozi shupavu aliye na misimamo thabiti isiyoyumbishwa hasa katika karne hii ya Utandawazi na Mitandao ya kijamii ambayo kwa asilimia kubwa baadhi ya watu wameitumia kama mwanya wa kupinga na kutoa taarifa potofu juu ya masuala mbalimbali.

Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Alphonce Temba amesema hayo baada ya kuona ishara njema kwa kile alichokiomba kwa Serikali kuwa, isaidie mchakato wa kuanza kwa Bandari Kavu Kwala (Vigwaza). Na kwa sasa ameona juhudi mpya.
Nakumbuka hivi karibuni niliweza kuandika na kutuma juu ya kuonekana kama kukwama kwa mradi mkubwa wa Serikali wa Bandari kavu Kwala ambao kimsingi umebeba malengo mengi kwa zaidi ya miaka mia moja ijayo ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kwa bandari kavu kunasaidia pia kutengenezwa fursa za kibiashara kwa wananchi zaidi ya elfu tatu, ukizingatia inaenda sambamba na reli ya mwendo kasi.Soma hapa kuhusu hoja ya awali ya Bandari Kavu Kwala>>>

Wasomi wengi na vijana wa kitanzania wanalo jukumu la kubuni kazi mpya zitakazozaliwa Kwala, pia wajenzi wanapata kazi mahoteli na kadhalika bila kusahau kuwa msongamano wa mabasi jijini Dar es Salaam unafikia mwisho ikizingatiwa nyakati za jioni wakati watu wanatoka makazini ndipo hapo hapo tulishuhudia msongamano mkubwa wa malori toka bandarini katika njia za Uwanja wa mpira wa Taifa, Buguruni mpaka Ubungo na Kimara.

Msongamano huo umekuwa na athari kadha wa kadha kiuchumi ikizingatiwa upotevu zaidi ya bilioni tatu kila siku za kazi upotea, achilia mbali safari za ndege watu wengi kuachwa na barabara kuchafuka na kuharibika kutokana na malori yanayofia njiani kwa matatizo mbalimbali kutiririsha oil chafu na kuharibu barabara, achilia mbali pia barabara za akiba kugeuzwa gereji bubu.

Mambo haya na mengine yamesababisha kilio kikubwa kwa wananchi kila kona hata baadhi ya wananchi kuendelea kuubeza mradi huo uliobuniwa muda mrefu na kuanza kazi mwaka 2017 kana kwamba ulikuwa umeingiliwa na wafanyabiashara wakubwa wa malori na kuhujumu ujenzi huo na kuanza kwa bandari kavu.

Kwani baadhi ya wananchi hasa madereva wanaosafiri nchi za Congo DRC na Zambia wamekuwa wakieleza vile wamekuwa wakitumia njia za vumbi katika nchi hizo zaidi ya kilomita mia moja katika baadhi ya migodi na magari ya nchi mbalimbali za Ukanda wa Kusini mwa Afrika yakibeba mizigo bila shida yoyote.

Leo Serikali ya Awamu ya Sita ambayo himo na ina sikio mpaka katika mitandao ya kijamii ni ya kupongeza sana, kwani ziara hii ya Rais wa Burundi nchini Tanzania imekuwa ni ishara njema ya kuufufua uchumi wa Tanzania kwa kushirikiana ma majirani zetu.


Hii ni kutokana na baada ya yale malalamiko tumeona rais anatembelea pamoja na maeneo mengine atakwenda kujionea fursa mpya ya eneo la kuifadhi mizigo la bandari kavu Kwala, wamekuja baadhi ya marais mbalimbali toka nchi mbalimbali, lakini hakuna aliyepata fursa aliyopewa Rais wa Burundi, Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye ya kufika katika bandari kavu ya Kwala.

Tena muda mfupi baada ya kutoa kilio kikubwa cha Bandari Kavu ya Kwala kuonekana kama imetelekezwa kutokana na juhudi za huko nyuma zilizokuwa zikisimamiwa kwa nguvu kubwa na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Awamu ya Tano, Mheshimiwa Izack Kamwele na kuutangazia umma mwezi wa kumi na mbili mwaka jana (2020) bandari kavu ilikuwa lazima ianze kazi.


Kwa taarifa zilizokuwepo Kwala ni kuwa mara baada ya kuondolewa mwanzilishi kiongozi wa Suma JKT Afande Kweka ndipo kila kitu kilidorora sana mpaka wakaja kuondolewa Suma ambao sasa wamerudishwa hii ni kutokana na kubadilisha uongozi na kumweka mtu ambaye akuwa amesoma mradi na changamoto za Kwala.

Napenda kutoa wito kwa watanzania kuendelea kutafuta fursa Kwala, Vigwaza, Chamakweza, Pingo na Chalinze kipindi hiki tuondokane na ile dhana ya kuona kuwa fursa za maisha na biashara zipo tu Dar es Salaam.

Pia nitoe wito wa wamiliki wa malori pamoja na uongozi wao ambao umekuwa ukilalamikiwa sana kwa kuwa wamekuwa na maslahi binafsi kutokana na wao pia kuwa wamiliki wa malori, wengi wakitamani wakati umefika viongozi wakuu wasiwe wamiliki wa malori ili kutoa fursa sawa ikizingatiwa kunakadiriwa kuwa na malori na matenki ya kusafirisha bidhaa hasa nje ya nchi zaidi ya elfu arobaini.

Ni wakati sasa wa kutafuta fursa za maegesho ya magari yao maeneo hayo, hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mheshimiwa Abubakar Kunenge alifanya mkutano katika Kata ya Vigwaza ambapo ni katika mwendekezo wa kufanya mikutano katika kata zote za mkoa wa Pwani pamoja na kusikiliza kero za wananchi, ambapo akijibu kero ya ulipwaji fidia ya njia ya Vigwaza kwenda Kwala kilomita 15 pamoja na mambo mengine akiambatana na viongozi wote wa idara na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo aliagiza halmashauri ya Chalinze kuharakisha kupima maeneo ya maegesho ya malori katika baadhi ya eneo lililotolewa kwa ajili ya bandari kavu ya Kwala kuanzia Vigwaza na kutoa wito kwa watu kuacha kuvamia mashamba ya watu.

Amesema, watachukuliwa hatua za kisheria, lakini Mheshimiwa mkuu wa mkoa alielezea kuwa umuhimu wa bandari kavu ni pamoja na kuondoa msongamano wa magari Dar es Salaam.
Mbali na mkuu wa mkoa na idara zake zote nimpongeze pia mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mstari wa mbele kuwaongoza na kuwasemea kwa mkuu wa mkoa juu ya kero mbalimbali za wananchi wake katika Kata ya Vigwaza na amekuwa mstari wa mbele kupigania kuanza kwa Bandari kavu ya Kwala akiamini wananchi wengi watapata ajira na mipango miji kufanyika kwa ajili ya upangwaji wa mji.

Hii ni fursa kubwa, kwani mpaka eneo la Gereza la mifugo Ubena Bwawani ambapo kutokana na sera mpya za Jeshi la Magereza Kujitegemea Mkuu wa gereza hilo, SSP Josephat Mkama ametoa fursa ya wadau mbalimbali kufika katika gereza hilo kwa ajili ya kupanga maeneo ya kiuchumi yakiwemo maegesho ya magari,viwanda, hoteli,maduka na vituo vya mafuta eneo hilo lenye urefu mkubwa zaidi ya kilomita 13.

Kwa msingi huo, Watanzania na wageni wanaalikwa kuwekeza pia gereza hilo lina fursa kadha wa kadha zikiwepo za mabwawa ya samaki na umwagiliaji, hivyo wapo tayari kutumia wafungwa kwa kuwapatia mahitaji yote wanayohitaji baada ya kuona wanavyozalisha, hivyo watanzania wasiogope Magereza kwa maana wamejipanga kuinua uchumi kwa kuzalisha kila kinachotakiwa na Watanzania.

Hivyo baada ya hoja yangu kutembea sana katika mitandao tunaona serikali wameliamulia kwa nguvu moja nasi tupo tayari kuisaidia kwa ajili ya kuisaidia nchi, lakini pia ikumbukwe kuwa utendaji wa bandari kavu Kwala utasaidia serikali iweze kuweka mfumo mzuri sana wa kukusanya mapato, kwa kuwa mzigo wote utakaoingia bandarini utanukuliwa wote na kutumwa Kwala ambapo utatolewa hapo, hivyo kutakuwa na ripoti mbili za bandarini na Kwala kwa idadi ya mzigo wote mwaka mzima, hivyo hata ukaguzi utakuwa mrahisi sana kiasi kuwa hakuna atakayeweza kuhujumu pesa za serikali kwa sababu ya historia ya mizigo zitasimamamiwa na mabosi wawili tofauti pamoja na vitengo vingine.

Achilia mbali na shirika la reli ambalo limekuwa likisuwasuwa kwa muda mrefu litapata fedha kwa kusomba mizigo yote ya ndani na nje ya nchi, faida kubwa kwa wateja wote ni gharama za kuhifadhi mizigo zitakuwa chini sana zaidi ya nusu ya kuhifadhi bandarini Dar es Salaam, hii ni kutokana na ukubwa wa eneo la Kwala, lakini tofauti ya gharama ya aridhi kati ya Dar es Salaam na Kwala.

Tunaomba sana mwaka huu kabla haujaisha mizigo ianze na minada Kwala bila kusahau mkadarasi ambaye inasemekana amesimama kazi kulipwa kama ajalipwa, hili amalizie kazi ya kuweka zege njia nzima kabla masika haijaanza.

Tunategemea Tanzania mpya ya maendeleo iliyotokana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mungu ibariki Tanzania na viongozi wetu wote.


Kwa ushauri wasiliana nami WhatsApp  +255755973787.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news