NA DOREEN ALOYCE
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abeli Makubi amesema jumla ya Shilingi Bilioni 466.781 (34%) zimetengwa kwenye Sekta ya Afya kwa ajili ya kutekeleza afua mbalimbali za afya nchi nzima.
Pia kati ya shilingi bilioni 466.781, Shilingi bilioni 259.228 zitasimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya utekelezaji wa miradi iliyoko chini ya Wizara ya Afya pamoja na taasisi na hospitali zilizo chini yake.
Akiongea leo na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu huyo amesema Shilingi Bilioni 207.643 zitasimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa ajili ya utekelezaji miradi ya afya iliyoko chini ya OR - TAMISEMI ikijumuisha vituo vya kutolea huduma za afya katika ngazi ya Msingi (Halmashauri) kuanzia hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati.
Amesema,Wizara ya Afya imeashaanza kutekeleza Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO - 19 kuanzia ngazi ya Taifa hadi Halmashauri.
MALENGO YA MIRADI KATIKA SEKTA YA AFYA, CHINI YA WIZARA YA AFYA
Amesema, katika kuimarisha huduma za dharura, wagonjwa mahtuti na wanaohitaji uangalizi maalum watatekeleza miradi itakayogharimu Shilingi bilioni 254.4.
"Uwekezaji huu unategemewa kupunguza vifo vya wagonjwa kwa asilimia 20-40% ndani ya vituo vya afya, kuimarisha huduma za maabara, mionzi na tiba mtandao itakayogharimu Shilingi bilioni 111.5. Hii itasaidia ugunduzi wa haraka wa magonjwa mbalimbali na kupunguza rufaa kwenda Hospitali ya Taifa," amesema Profesa Makubi.
Na kuongeza "Kuimarisha huduma za chanjo dhidi ya UVIKO - 19 na elimu ya afya kwa umma dhidi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo; itakayogharimu Shilingi bilioni 43.2. Hivyo tutaweza kuwakinga wananchi wengi dhidi ya vifo vinavyohususiana na UVIKO-19. Kuimarisha miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za afya itakayogharimu Shilingi bilioni 41.8 na hivyo kupanua na kuboresha huduma za kibingwa katika ngazi ya mikoa na Kanda.Kufanya tafiti za kitaalam kuhusu Virusi vya Korona pamoja na kuwajenga uwezo watoa huduma za afya; itakayogharimu Shilingi bilioni 15.9. 2.1.," amesema.
NAMNA MALENGO YANAVYOTEKELEZWA
Amesema, katika kuimarisha huduma za dharura, wagonjwa mahtuti na wanaohitaji uangalizi maalum; Shilingi bilioni 254.4. Sekta imeaza michakato ya kukarabati na kujenga majengo ya matibabu ya dharura (EMD) 102; vitengo vya wagonjwa wanaohitaji uangallizi maalum (ICU) 67 na kusimika vifaa vyake.
" Hospitali ya Taifa itakarabati ICU 2, Hospitali Maalum na Ubingwa Bobezi (ICU 5 na EMD 1),Hospitali za Kanda (ICU 5 na EMD 4),na katika ngazi ya mikoa na Halmashauri (ICU 30 na EMD 80) chini ya OR TAMISEMI".
Kuimarisha mfumo wa rufaa kwa kununua na kusambaza magari 253 ya kubebea wagonjwa, kati ya magari hayo magari 20 ‘advanced ambulances’ yatapelekwa katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere (1), KIA (1), Mwanza Airport (1), Hospitali ya Mzena (1), Hospitali za Rufaa za Mkoa (8), Hospitali za Kanda (6), Hospitali Maalum na Ubingwa Bobezi (5). Magari 233 ni ya kawaida (basic ambulances) na yatapelekwa Hospitali za Rufaa za Mkoa (38) na magari 185 katika ngazi ya OR TAMISEMI.
Fedha hizo zinatokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupambana na madhara ya UVIKO-19 zimewezesha nchi kupata mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Kimarekani milioni 567.25 sawa na Shilingi trilioni 1.362 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kama mlivyosikia tarehe 10/10/2021 wakati Mhe. Rais.