Rais Dkt.Mwinyi alivyopania kuwapa tabasamu kubwa wajasiriamali wote

Na Rajab Mkasaba

“Tutawasajili wajasiriamali wote na kuwapatia vitambulisho. Pia, tutatoa mafunzo ya namna bora ya kuitumia mitaji na mikopo hiyo katika kupata vifaa na zana za kisasa na kuendesha shughuli za ujasiriamali kitaalamu zaidi, kulingana na mahitaji ya masoko ya wakati tulio nao;
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Kitambulisho Mjasiriamali kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Bi.Amina Said Mdoe, hafla hiyo ya kuwakabidhi Vitambulisho Wajasiriamali Wadogo ilifanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar hivi karibuni.(Picha na Ikulu).

Hayo ni maelezo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika sehemu ya hotuba yake ya uzinduzi wa Baraza la 10 la Wawakilishi mnamo Novemba 11, 2020.

Rais Dkt. Mwinyi tokea anaingia madarakani na hata katika kampeni zake zote alizozifanya wakati akigombea nafasi ya Rais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alikuwa akisisitiza azma yake ya kuwasaidia na kuwaunga mkono wajasiriamali wakiwemo wajasiriamali wadogo wadogo.

Aidha, katika ziara zake alizozifanya hivi karibuni katika mikoa na wilaya zote za Unguja na Pemba, Rais Dkt. Mwinyi alikuwa akisisitiza na kueleza kwamba azma yake ya kuwasaidia wajasiriamali ikiwa ni pamoja na kuwasajili na baadae kuendelea na taratibu za kuwasaidia kupata elimu ya ujasiriamali, mtaji wa kuendeshea shughuli zao pamoja na masoko ya kuulia bidhaa zao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Kitambulisho Mjasiriamali kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, Bi.Fatma Khamis Juma, hafla hiyo ya kuwakabidhi Vitambulisho Wajasiriamali Wadogo ilifanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitambulisho chake na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Masoud Ali Mohammed, baada ya kukizindua na kuwakabidhi wajasiriamali wadogo wa Unguja na Pemba, hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizindua Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar na (kulia kwa Rais) ni Waziri wa Nchi Afisi ya RaisTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe.Masoud Ali Mohammed na (kushoto kwa Rais) ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe Mustafa Idrisa Kitwana na Mwenyekiti wa CCMMkoa wa Mjini Kichama.Ndg Talib Ali Talib.(Picha na Ikulu).

Pia, katika ziara zake hizo za Mikoa aliahidi kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wakati akizungumza na wananchi akiwa Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mkoani eneo la bandarini katika Mkoa wa Kusini Pemba ambapo pia katika hotuba zake za majumuisho katika mikoa yote aliagiza kwa Mabaraza ya Manispaa na Halmashauri kwa kushirikiana na Uongozi wa Wilaya, Mikoa na Wizara ya TAMISEMI kwa jumla kuwa na mipango na mikakati madhubuti ya kuwawekea wajasiriliamali maeneo maalum wanayoweza kufanyia shughuli zao bila ya bughudha na usumbufu wowote.

Hivyo katika kuhakikisha anatekeleza ahadi yake hiyo aliyokuwa akiahidi mara kwa mara, Rais Dkt. Mwinyi hivi karibuni alizindua vitambulisho vya Wajasiriamali na kusema kuwa vitambulisho hivyo vina umuhimu katika kurasimisha shughuli zao, pamoja na kuwatambua kisheria kuwa ni miongoni mwa wachangiaji wa uchumi.  

“Kwa hakika leo tunafungua ukurasa mpya wa jitihada za Serikali katika malengo yetu ya kuyaimarisha mazingira ya kufanyia kazi ya wajasiriamali wetu. Katika ziara ya Mikoa na Wilaya zote za Zanzibar niliyoifanya hivi karibuni, niliahidi kuwa suala la kuwapatia vitambulisho maalum wajasiriamali wadogo wa Zanzibar na kuwaondolea tatizo la kulipa tozo kila mwezi au kila siku ni moja ya vipaumbele vya Serikali,”alieleza Rais Dkt. Mwinyi katika hotuba yake hiyo ya uziduzi wa vitambulisho vya Wajasiriamali..

Katika hotuba yake hiyo aliyoitoa huko katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni Zanzibar Rais Dkt. Mwinyi alieleza kwamba mbali ya hatua hizo pia, kuwepo kwa vitambulisho hivyo kutawarahisishia Wajasiriamali hao kupata huduma mbali mbali zikiwemo za kupata mikopo katika taasisi kadhaa za kifedha zikiwemo benki.
Wajasiriamali Wadogo kutoka Unguja na Pemba wakimsikiliza Raiswa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi.(hayupopichani) wakati akiwahutubia katikahafla ya Uzinduzi wa Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo Zanzibar, uliofanyikakatika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati akiwahutubia Wajasiriamali Wadogo Zanzibar katika hafla ya Uzinduzi wa Vitambulisho vya Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Andulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Alisema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa pamoja na kuzingatia matakwa ya sheria mbali mbali zinazohusiana na wajasiriamali ambapo lengo lake ni kuweka mazingira maalum ya kuyasaidia makundi ya wajasiriamali wakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia, alieleza malengo ya Serikali ya Awamu ya Nane ya kutoa Bilioni 100 kwa ajili ya kwuasaidia Wajasiriamali ambapo Serikali itatoa Bilioni 50 na Benki zilizoamua kuwasaidia Wajasiriamali zitatoa Bilioni 50 ambazo fedha hizo zitatumika kwa kuwatafutia mafunzo, mitaji pamoja na masoko..

Pamoja na hayo, Rais Dk. Mwinyi aliwahakikishia Wajasiriamali kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina dhamira ya dhati ya kuwajengea mazingira bora ya kufanya shughuli zao Wajasiriamali Wadogo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanajengewa maeneo maalum ya kufanyia kazi.


Wajasiriamali Wadogo kutoka Unguja na Pemba wakimsikiliza Raiswa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupopichani) wakati akiwahutubia katikahafla ya Uzinduzi wa Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo Zanzibar, uliofanyikakatika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa tayari Serikali imeshaanza mazungumzo na wawekezaji katika kufanikisha ujenzi wa masoko kwa kila Wilaya Unguja na Pemba huku akitumia fursa hiyo kutoa taarifa njema kwamba katika kipindi kifupi kijacho Serikali itaanza ujenzi wa masoko katika eneo la Jumbi na Chuini kwa Nyanya.

Vile vile, hakuchelea kueleza kwamba Serikali ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo ya ujenzi katika eneo la Darajani eneo ambalo litakuwa na sura mpya na fursa nyingi zaidi kwa wafanyabiashara wadogo kufanya biashara zao kwa ufanisi

“Kwa hakika leo tunafungua ukurasa mpya wa jitihada za Serikali katika malengo yetu ya kuyaimarisha mazingira ya kufanya kazi ya wajasiriamali wetu”,alisema Rais Dk. Mwinyi.

Sambamba na hayo, aliwapongeza Wajasiriamali wote waliokwisha jitokeza kujisajili tokea kuanza kwa zoezi hilo na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wale wote ambao hawajasajili kufanya hivyo katika vituo vilivyoandaliwa.

Pia, aliwahimiza Wajasiriamali wote kuitumia fursa hiyo kujisajili na kufuata taratibu zote ikiwemo kufanya kazi zao katika maeneo yaliyoruhusiwa na kuzingatia kuweka usafi kwa kushirikiana na Mabara ya Miji, Manispaa na Halmashauri zote.

Aliupongeza uongozi na Watendaji wa Kampuni ya AIM GROUP LIMITED kutoka Dar-es-Saalam kwa kazi nzuri ya utayarishaji wa mfumo wa usajili wa Wajasiriamali wadogo Zanzibar ambao leo umezinduliwa rasmi na kuwawezesha Wajasiriamali kupata vitambulisho vyenye ubora

Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ni miongoni mwa malengo ya Serikali ya Awamu ya Nane katika kukabiliana na tatizo la umaskini wa kipato unaosababishwa na ukosefu wa ajira, Serikali inatambua kuwa bado kuna changamoto zinazowakabili wananchi katika kuendesha shughuli za ujasiriamali, ambazo zinahusiana na ukosefu wa mitaji, vifaa, utaalamu wa kutosha wa kuendesha biashara na utafutaji wa masoko ya uhakika ya kuuzia biashara hizo.

Katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali itauimarisha Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kuuongezea uwezo wa kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi wengi zaidi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Kitambulisho Mjasiriamali kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ndg.Suleiman Mbarouk Mohammed, hafla hiyo ya kuwakabidhi Vitambulisho Wajasiriamali Wadogo iliofanyika katika ukumbi waSheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Aidha, tutawajengea wajasiriamali sehemu maalum za kufanyia biashara zao zitakazojengwa vizuri, ili waondokane na usumbufu wa kuhamahama huku na kule ambapo pamoja na jitihada hizi, Serikali itawawekea mfumo na utaratibu bora wa kulipa kodi mara moja tu kwa mwaka na kuondosha ile kero ya utitiri wa kodi.

Katika kuhakikisha kwamba mkakati huu unaleta ufanisi unaoutarajiwa, Serikali itafuatilia kwa karibu na kufanya tathmini ya mikopo inayotolewa katika vikundi ili kujiridhisha endapo inawafikia walengwa na kwamba hakuna matumizi mabaya ya fedha hizo yanayofanywa na watumishi wa Serikali wasio waaminifu.

Serikali ina dhamira ya dhati ya kuwajengea mazingira bora ya kufanya shughuli Wajasiriamali ambapo malengo ya Serikali ni pamoja na kuhakikisha Wajasiriamali Wadogo wanajengewa maeneo maalum ya kufanyiakazi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati akiwahutubia Wajasiriamali Wadogo Zanzibar katika hafla ya Uzinduzi wa Vitambulisho vya Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Andulwakil KikwajuniZanzibar.(Picha na Ikulu).

Kwa maelezo ya Rais Dkt. Mwinyi tayari Serikali imeshaanza mazungumzo na wawekezaji katika kufanikisha ujenzi wa masoko kwa kila Wilaya Unguja na Pemba. Aidha, napenda nikupeni taarifa njema kwamba katika kipindi kifupi kijacho Serikali itaanza ujenzi wa masoko katika eneo la Jumbi na Chuini Kwa Nyanya.

Vile vile, Serikali ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo ya ujenzi katika eneo la Darajani Mjini Zanzibar eneo ambalo litakuwa na sura mpya na fursa nyingi zaidi kwa wafanyabiashara wadogo kufanya biashara zao kwa ufanisi. “Kwa kweli nimefarajika kwa nini na Kibandamaiti tusijenge soko la kudumu”,alisema Dk. Mwinyi.

Pamoja na hatua ya ujenzi wa miundombinu ya masoko, Serikali inaendelea na utekelezaji wa dhamira yake ya kuiunganisha mifuko ya uwezeshaji ili kuwa na Mfuko mmoja imara ambao utaweza kuratibu kwa ufanisi mkubwa shughuli za utoaji wa mikopo nafuu kwa wananchi wakiwemo wajasiriamali wadogo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mjasiriamali kutoka Soko laKibandamaiti Bi.Hawa, alipotembelea mabanda ya maonesho ya Wajasiriamali Wadogo, wakati wa uzinduzi wa Vitambulisho vya Biashara kwa Wajasiamali Wadogo waUnguja na Pemba, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Lengo la Serikali ni kukabiliana na changamoto zilizokuwepo katika mifuko iliyopo ikiwemo Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Mfuko wa Kusaidia uendelezaji wa Viwanda Vidogo vidogo (SMIDA), Mfuko wa Vijana, mfuko wa walemavu, pamoja na tatizo la upatikanaji wa asilimia 10 ya mapato ya Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya kwa ajili ya makundi ya kinamama, vijana na watu wenye ulemavu. 

Serikali ya Awamu ya Nane haitotosheka kutoa mikopo na mitaji na baadae kuripoti takwimu za vikundi vilivyopokea mikopo hiyo, na kuirejesha au kutoirejesha na badala yake juhudi za makusudi zitachukuliwa katika kuhakikisha mikopo hio imeleta faida kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news