Rais Dkt.Mwinyi aongoza dua maalum ya Hitma

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo amewaongoza Waumini wa dini ya Kiislamu katika dua maalum ya Hitma iliyosomwa huko katika Msikiti wa Ijumaa, Mkwajuni Kidombo, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitia ubani kuashiria kuanza kwa dua Maalum ya kisomo cha hitma kuwaombea waliotangulia mbele ya haki, dua iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mkwajuni Kidombo, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa, (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla (kushoto kwa Rais) Mtoto wa Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Tano Alhaj. Dk.Salmin Amuor Juma.Ndg.Amini Salimin Amour.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkwajuni Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja katika kisomo na dua Maalum kuwaombea Waliotangulia mbele ya haki, iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo, dua hiyo inayokwenda sambamba na Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman na (kushoto kwa Rais) Ndg. Amini Salimin Amour, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj.Othman Masoud Othman, Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj. Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu).

Dua hiyo inayokwenda sambamba na Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) ni utamaduni wa muda mrefu uliowekwa na wakazi wa kijiji hicho ambapo kila ifikapo mwezi kama huu wa Mfunguo Sita hufanyika hafla hiyo ambayo huwakusanya wanakijiji wa eneo hilo pamoja na wale wa maeneo jirani wakiwemo wenye asili ya Kijiji hicho wanaoishi Mjini kwa ajili ya dua na Maulid hayo.
Wananchi wa Mkwajuni Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika dua Maalum na kisomo cha Hitma iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo, inayokwenda sambamba na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) hufanyika kila mwaka.(Picha na Ikulu).

Katika dua hiyo iliyosomwa katika Msikiti wa Ijumaa Mkwajuni Kidombo, viongozi mbalimbali wa dini, vyama vya siasa na Serikali pamoja na wananchi walihudhuria akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na viongozi wengine wakiwemo wastaafu.

Mapema akisoma hotuba ya Ijumaa Sheikh Mussa Haji Makame alieleza dhamira ya Mwenyezi Mungu kumleta duniani Mtume Muhammad (S.A.W) ikiwa ni kuja kubainisha haki na kukataza maovu sambamba na kuufunza umma namna ya kuzitekeleza haki hizo pamoja na malipo yake. Rais wa Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akimsalimia Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Alhaj Dk.Salmin Amour Juma, alipofika nyumbani kwake Kijijini Kwao Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakati wa hafla ya Kisomo cha Dua Maalum iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo na (kushoto ) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Husseinn Ali Mwinyi, baada ya dua hiyo inayokwenda na sambamba na Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad.(S.A.W) hufanyika kilia mwaka katika Kijiji cha Kidombo Mkwajuni Unguja.(Picha na Ikulu), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume.(hayupo pichani) na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Alhaj Dk.Salimini Amour Juma, Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj.Ali Hassan Mwinyi na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Alhaj Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakiitikia dua hiyo, baada ya kumaliza kumsalimiana kumjulia hali nyumbani kwake Kijiji cha Kidombo Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu).

Wakati huo huo, Alhaj Dk. Mwinyi aliungana na viongozi wengine kwenda kumsalimia na kumjuulia hali Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Tano, Alhaj Dkt. Salmin Amour Juma hapo nyumbani kwake kijijini kwao Mkwajuni Kidombo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news