NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Simba SC imejizolea alama tatu kwenye mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC.
Ni baada ya kuwafunga Polisi Tanzania bao 1-0 katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao timu zote zilikuwa zinashambulia kwa kushtukiza zilikwenda mpaka mapumziko zikiwa hazijapata bao lolote.
Polisi Tanzania ambayo imeanza ligi vizuri, mechi zake zote tatu ilifanikiwa kupata ushindi na kuweza kuongoza ligi hiyo ambayo kwa sasa imekuwa ya ushindani kutokana na timu zote kuonekana kujiandaa vema.
Wekundu wa Msimbazi walifanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa ambapo yalizaa matunda, kwani kuingia kwa Benard Morrison kulionesha timu kuhitaji muda wote kupata goli hasa kwa kulisakama goli la wapinzani kwa nguvu.
Morrison alichezewa rafu dakika ya 86 ya mchezo hivyo mwamuzi akaamuru kuwekwe mkwaju wa penati ambao ulienda kupigwa na kiungo Mzambia, Larry Bwalya na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo.
Tags
Michezo