NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) iliundwa kwa Sheria ya Nguvu za Atomu Na. 7 ya Mwaka 2003 (Atomic Energy Act No.7 of 2003).Sheria ya Bunge Na. 7(2003) ilifuta Sheria Na.5 ya mwaka 1983 (The Protection from Radiation, No. 5 of 1983) iliyoanzisha Tume ya Taifa ya Mionzi (National Radiation Commission).
Sheria hii imeipa TAEC mamlaka ya kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini ikiwemo kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia nchini.

Pichani juu ni fundi mwandamizi Bw. Eusebio Kitosi akifanya matengenezo ya Mashine ya X-Ray (Philips MRS) ya Hospitali ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu. (Picha zote na TAEC).Jifunze pia kuhusu TAEC hapa>>>