NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Mwinyi leo Oktoba 25, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu na kueleza haja kati ya Zanzibar na Kenya kuendeleza ushirikiano na uhusiano uliopo hasa katika sekta ya biashara na uwekezaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu wakati wa mazungumzo yao alipofika Ikulu jijini Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania, Mhe.Dan Kazungu wakati wa mazungumzo yao alipofika Ikulu Jijini Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo viongozi hao kwa pamoja walisisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kuimarisha sekta hizo hasa ikizingatiwa kwamba pande mbili hizo zina uhusiano mwema pamoja na kuwepo vyanzo ya mashirikiano katika sekta hizo za uchumi.
Rais Dkt.Mwinyi alisisitiza haja ya kurasimishwa kwa biashara na kuwekewa mazingira mazuri ya bandari na vyombo vya usafiri kwa wafanya biashara wa pande mbili hizo ili kuweza kufanya biashara zao vizuri hasa ikizingatiwa ukaribu uliopo baina ya Zanzibar na Kenya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimkabidhi zawadi ya mlango mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Tanzania, Mhe.Dan Kazungu baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipokea picha ya kuchora inayoonyesha Uchumi wa Buluu kupitia Uvuvi kutoka wa mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Tanzania, Mhe.Dan Kazungu baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu jijini Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na mgeni wake Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania, Mhe.Dan Kazungu baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu jijini Zanzibar leo. (Picha zote na Ikulu).
Viongozi hao pia, walieleza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kihistoria wa utamaduni uliopo baina ya Kenya na Zanzibar ambao unahitaji kuendelezwa na kuimarishwa zaidi ili uweze kuleta manufaa kwa pande mbili hizo.