NA MWANDISHI MAALUM
Timu ya taifa ya Tanzania ya wasichana chini ya umri wa miaka 20 imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu ya michuano ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la mwakani baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Eritrea, Oktoba 9, 2021 katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Mabao ya Tanzanite yamefungwa na Irene Kisisa na Protas Mbunda na kwa matokeo hayo wanakwenda Raundi ya Tatu kwa ushindi wa jumla wa 5-0 kufuatia kuwachapa Eritrea 3-0 kwenye mechi ya kwanza Septemba 25 jijini Asmara.
Kwa msingi huo, Tanzania itamenyana na Burundi katika mfululizo wa kuwania tiketi ya fainali za Costa Rica Agosti mwaka 2022.
TWIGA STARS
Wakati huo huo,timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imefanikiwa kutwaa ubingwa wa COSAFA baada ya kuichapa Malawi 1-0 jioni ya Oktoba 9, 2021 Uwanja wa Nelson Mandela Bay jijini Port Elizabeth nchini Afrika Kusini.
Mfungaji wa bao pekee la Twiga Stars ni Enekia Kasonga dakika ya 64, mchezaji wa Alliance ya Mwanza ambaye hivi karibuni klabu yake imeripotiwa kumuuza Morocco.
Tags
Michezo