NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi jana aliwaongoza waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na viongozi na wafanyakazi wa “VIGOR A TURKY’S GROUP OF COMPANIES”, katika Maulid ya kuadhimisha Kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyoandaliwa na Makampuni hayo na kufanyika huko katika viwanja vya kiwanda cha Zainab Bottles, Mombasa Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali na wa Kampuni ya Vigor, wakati akiwasili katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad ( S.A.W) yaliyofanyika jana usiku.
Sherehe hizo za Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambazo hufanywa na “VIGOR A TURKY’S GROUP OF COMPANIES”, kila mwaka pia, zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini na Serikali akiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih.
Kwa mujibu wa maelezo ya uongozi wa “VIGOR A TURKY’S GROUP OF COMPANIES”, Sherehe hizo za Maulid zilizanzishwa na Marehemu Salim Hassan Turky ambaye ndiye aliyekuwa muasisi wa Maulid hayo ambaye pia, alikuwa Mwenyekiti wa “VIGOR A TURKY’S GROUP OF COMPANIES”,.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya ufunguzi wa Maulid ya kuadhimisha Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Bw. Multaza Turky na (kushoto kwa Rais) Mhe Toufiq Turky Mwenyekiti wa Makampuni ya Vigor A Turky Group, wakitikia dua,hafla hiyo imefanyika katika kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B”Unguja jana usiku.
Usadhi Sayyid Abdulrahaman Al Habshy akisoma Quran Suratul Yasin wakati wa hafla ya Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yalioandaliwa na Kampuni ya ‘Vigor A Turky Group of Companies’ yaliofanyika jana usiku 26-10-2021 katika viwanja vya kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Wanafunzi wa Madrasatul Noor Islamiya wakisoma Qaswida ya Yarabbi Swalli wakati wa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yalioandaliwa na Kampuni ya Vigor A Turky’s Group of Companies katika viwanja vya kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Ustadhi Halfan Amran akisoma Mlango wa kwanza wakati wa hafla ya Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika Qiyaam wakati ukisomwa mlango wa nne wa Maulid ya Barzanj kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) akiwa mgeni rasmin katika Maulid hayo yalioandaliwa na kampuni ya Vigor A Turky’s Group Companies, yaliofanyika katika viwanja vya kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na (kushoto kwa Rais) Mhe Taufiq Turky na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali.
Sayidd Maalim Abubakar Bin Said akisoma akisoma dua ya barzazanji wakati wa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad(S.A.W) yalioandaliwa na kampuni ya Vigor A Turky’s Group Companies , yaliofanyika katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Kiwanda cha Zainab Bottles Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.(Picha na Ikulu).
Mbali ya Maulid hayo pamoja na nasaha zilizotolewa juu ya umuhimu wa kumsalia Mtume Muhammad (S.A.W) sambamba na kufuata nyayo zake, hadhara iliyokuwepo katika Maulid hayo pia, ilitumia fursa hiyo kumuombea dua Muasisi wa Maulid hayo Marehemu Salim Hassan Turky, ndugu, jamaa, viongozi pamoja na Waislamu wote, dua iliyoongozwa na Sheikh Maalim Ali Hamed Jabir.
Pamoja na hayo, uongozi wa Makampuni hayo hiyo chini ya Mwenyekiti wake Taufiq Turky uliahidi kuyaendeleza yale mema yote yaliyoachwa na Muasisi huyo huku akimuhakikishia Alhaj Dk. Mwinyi kwamba “VIGOR A TURKY’S GROUP OF COMPANIES”, itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar sanjari na kuziunga mkono juhudi za Rais Dk. Mwinyi za kuwaletea maendeleo Wazanzibari wote.